Fomu za talaka zijazwe online

Fomu za talaka zijazwe online

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Nina hoja.

Ili kupunguza visa vya Wanandoa kuendelea kuwekeana chuki na kuumizana wakati wa mchakato wa kutengana kimahakama, naona ni vema fomu za TALAKA ziwekwe kwenye mifumo ya mahakama mtandaoni ili watalaki wawe wanajaza huko.

Ikiwezekana maamzi yawe yanatolewa kupitia mifumo salama ya mawasiliano ya wahusika.

Jioni njema ndugu zangu. Kesho ni jumapili.📻
 
Hahah, nimewaza umekutana na jambo gani lakini naona umekwazika na jambo katika mchakato wako wa ama kudai au kudaiwa Talaka.

Pole Mkuu

Nikirudi kwenye hoja yako, kama ni swala la kiusalama ipo mamlaka, jeshi la polisi na Mahakama yenyewe.

Fomu kujazwa online inawezekana ila mfumo bado haujaanza kazi kikamilifu japo sio kujaza bali kuwasilisha online na kuendesha kesi online.

Tuipe Mahakama muda pengine mwaka 2024 ukawa mwaka rasmi wa Mahakama Mtandao Tanzania.
 
This is a good idea na nida number should be involved na message inatumwa kwa muhusika na. File number for review then mnapeleka id kwa mahakama it’s done
 
Hahah, nimewaza umekutana na jambo gani lakini naona umekwazika na jambo katika mchakato wako wa ama kudai au kudaiwa Talaka.

Pole Mkuu

Nikirudi kwenye hoja yako, kama ni swala la kiusalama ipo mamlaka, jeshi la polisi na Mahakama yenyewe.

Fomu kujazwa online inawezekana ila mfumo bado haujaanza kazi kikamilifu japo sio kujaza bali kuwasilisha online na kuendesha kesi online.

Tuipe Mahakama muda pengine mwaka 2024 ukawa mwaka rasmi wa Mahakama Mtandao Tanzania.
😀😀😀 Hakuna lililonikuta mkuu ila siku kadhaa zimepita nilishuhudia vurugu kubwa sana kwenye maeneo ya mahakama baada ya mwanamke mtalakiwa kuongozana na kidume mpya mahakamani.
 
Back
Top Bottom