Zamani kulikuwa na 2 points system kwa mshindi na poit 1 kwa sare, FIFA walibadili nadhani katika Kombela dunia mwaka 94 kule USA, kwa vile Fifa waliona pointi 3 zitaleta motisha kwa timu kutafuta ushindi kwa vile zawadi ni mara 3 zaidi ya sare na hii ni katika jitihada za kuongeza ushindani, kwani endapo timu zitakuwa sare 0-0 dakika za mwisho kutakuwa na pressure kwa timu zote mbili kupata killer goal ili kuzoa pointi 3, na timu inapokuwa imefungwa mfano 1-0 watajitahidi kusawazisha ili kutopoteza pointi 3.
Waingereza wao walianza na hii system mapema katika ligi yao ya 1981.
Kwa kweli ukiangalia kwa mfano hapo zamani ukicheza mechi 4 na kushinda 3 na sare 1 unaambulia pointi 7 wakati sasa utakuwa na pointi 10, hii inapelekea timu ku-focus zaidi kwenye ushindi kwa vile it is more rewarding.