Valid_Options
Member
- Nov 13, 2010
- 43
- 0
Au kwa kifupi unapodroo mfululizo inakula kwako zaidi kwenye 3 points system kuliko kwenye 2 points system...sijajua kwa nini FIFA waliamua kubadili toka kwenye 2 points kuja kwenye 3 points
Nakukubali sana unajua soka na unafuatilia toka siku nyingi,nakumbuka hata bongo nao ilikuwa hivyo hivyo hadi 1994 nao wakaanza kushinda ni pointi 3,ila kuna kitu sitosahau bongo viongozi hawajui sheria za soka na jinsi ya kupanga msimamo,mathalani zamani ilikuwa bongo wao wanaangalia magoli ya kufunga ikiwa point mpo sawa hawakujua kabisa kitu kinaitwa goal difference,asante sana DTV kuanza kuonyesha ligi ya England miaka ya 1995 au 1996 nadhani ndio wakaanza kuangalia goal difference,mana kuna mwaka timu fulani,sitaji jina,walipewa ubingwa eti magoli ya kufunga ni mengi kuliko mwenzie,lakini ukiangalia walikuwa pointi sawa,yule alikuwa na magoli ya kufunga 40 ya kufungwa 38,mwenzake alikuwa na ya kufunga 35 ya kufungwa 22,ukiweka goal difference yani ya kufunga toa ya kufungwa yule wa mwanzo niliemuorodhesha ni 40-38 unapata 2,mwingine 35-22=13,lakini ubingwa alipewa yule mwenye goal difference 2 sio wa 13,kisa alikuwa na magoli mengi ya kufunga,ila kwa nchi kama Spain wao wanaangalia mechi baina yenu mlivyokutana baada ya mechi zote 2 mlizocheza home and away mwenye rekodi nzuri eg yani kama mtoano inakuwa ndio anakuwa juu,hata UEFA nayo wanatumia sheria hii,na world cup ktk bara la Afrika na CAF pia wanatumia hii sheria,ndio ilimnyima Nigeria nafasi ya kwenda Germany 2006,alimzidi Angola magoli pamoja na Goal Difference ila walipokutana wao kwa wao,Nigeria alishinda 1-0 kwao na Angola alishinda 2-0 kwao kwahiyo ikawa Angola 2 Nigeria 1 kwa jumla kwahiyo ikamnufaisha Angola kuingia World Cup.Zamani kulikuwa na 2 points system kwa mshindi na poit 1 kwa sare, FIFA walibadili nadhani katika Kombela dunia mwaka 94 kule USA, kwa vile Fifa waliona pointi 3 zitaleta motisha kwa timu kutafuta ushindi kwa vile zawadi ni mara 3 zaidi ya sare na hii ni katika jitihada za kuongeza ushindani, kwani endapo timu zitakuwa sare 0-0 dakika za mwisho kutakuwa na pressure kwa timu zote mbili kupata killer goal ili kuzoa pointi 3, na timu inapokuwa imefungwa mfano 1-0 watajitahidi kusawazisha ili kutopoteza pointi 3.
Waingereza wao walianza na hii system mapema katika ligi yao ya 1981.
Kwa kweli ukiangalia kwa mfano hapo zamani ukicheza mechi 4 na kushinda 3 na sare 1 unaambulia pointi 7 wakati sasa utakuwa na pointi 10, hii inapelekea timu ku-focus zaidi kwenye ushindi kwa vile it is more rewarding.