Hahaa, we kubali tu nimekushitukia!!
Hongera Lizy kwa kutaka kubanana na mpenzio mbele ya screen, ila chunga tu usichukue tabia za mwanaume anapoangalia mpira;
Mfano, mchezaji anaweza akachemsha uwanjani, ukasikia mwenzako anasema maneno ambayo humsikii akiyasema kila siku lol!
Mwanakwetu kaeleza vizuri tu. Ila kuna sheria moja inayosema kwamba timu lazima iwe na wachezaji atleast 7 uwanjani ili mchezo uendelee. Hii haitokei mara kwa mara. Mfano kocha katumia wachezaji wote 3 kama substitute. Anakuwa hana wachezaji wa kuongeza. Halafu itokee wachezaji 5 waumie au wapate kadi nyekundu, watabaki wachezaji 6 uwanjani. Basi refa anaweza kuahirisha mchezo, na chama cha mpira kikaamua mshindi ni nani kutokana na yaliyotokea. Hii sikumbuki mara ya mwisho imetokea wapi. Ila sheria hiyo ipo.
Afadhali umekuja kuuliza hapa, maana ukimwuliza wakati anaangalia unamkatisha concentration, halafu maswali mengine anaweza kupuuzia. Kwa mfano unaweza uliza;
1) Hivi Thierry Henry si anachezea Arsenal? Sasa anafanya nini Barcelona au timu ya Taifa ya Ufaransa?
2) Jamani David Beckham handsome, lakini bukta haimpendezi. hivi hawezi kucheza na surualli ya D&G?
3) Hivi kwanini golikipa anatumia mikono wengine hawatumii? Mbona hapigwi penalti?
4) Hivi kwanini mababa 22 yanakimbiza kampira kamoja? Kwani wamechizika? (DONT TRY THIS....YOU are insulting a man's intelligence hahaaa).
Questions like these are bad for your health!! Nikifikiria mengine nitakwambia!LOL.
Ila ni vizuri unamfikiria. Pia usimtume akafanye shopping wakati mechi imekaribia kuanza au katikati ya mechi. Akisema atafanya ujue atafanya.
Hakikisha umetayarisha vitafunio wakati wa mechi, ili hasira zikimzidi, mpatie tissue na vitamutamu, anameza na kujipangusa. Hata ikibidi mpe massage ya kichwa, maana kuangalia mpira si mchezo.
Fuata masharti haya, utapendwa mpaka uishiwe nguvu....LOL!!