Footsprints ni nini na zinaondolewaje?

Footsprints ni nini na zinaondolewaje?

Chamoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
8,577
Reaction score
18,774
Footsprints ni nini na zinaondolewaje?

Footprints (kwenye mtandao) inamaanasha alama zinazoachwa kwenye
mtandao. Mfano unapo tumia bao bonye (keyboard) kuchapa jina lako
kwenye tovuti (website) hii ya JF hiyo ni footprint.

Sasa hebu tuseme jina lako ni "sikujui Mkopachuma" na mimi nimeamua
kuvuna (harvesting) tovuti zote ambazo zina jina "sikujui Mkopachuma"
ninaweza kutangeneza ka-programu (scraper) ambako kata tafuta orodha
ya hizo tovuti kutoka google, yahoo au bing.

Unaweza kuniuliza kwa nini nitafute hilo jina?... Sababu zina weza kuwa
nyingi, mojawapo inaweza kuwa jina "sikujui Mkopachuma" linaambatanishwa
na jambo fulani ililotokea wiki iliyo pita ambapo ilibainika... hiyo binti alikuwa
anatembea na kigogo mmoja pale Dar.

Sasa kama mimi ni huyo kigogo na ninataka kuwachimba hao wambea walio
nianika ili niwafanyie nitatengeneza hiyo scraper ambayo kwa kutumia kanuni
fulani (certain rules/instructions) nitaweza kufuata footprints ili niweze kupata
hizo tovuti zilizo nianika.

Mpaka sasa mambo murwa... sasa hii ni hadithi tuu ila nilikuwa nataka
uelewe footprint ni nini.

Kuhusu "email footprint" ni kwamba kuna watu ambao huwa wanavuna
emails ili waweze ku spam kama walivyo mfanya jamaa yetu (hawa jamaa
huwa wana vuna mamilioni ya emails). Sasa hawa watu huwa wanatafuta
mfumo huu "maneno_fulani_au_namba@tovitu.com" huu ni mfumo ambao
unaweza kuvuna emails. wanatumia kitu kinaitwa regular expression, kama
hii \b[A-Z0-9._%-]+@[A-Z0-9.-]+\.[A-Z]{2,4}\b

Hiyo kanuni ya regex (regular expression) itatafuta emails zote zilizo acha
footprint kwenye toviti mbalimbali.

Sasa swali lako la "zinaondolewaje"... ni kwamba wakati unalambaza
(surfing) kwenye tuvuti mbalimbali na ukawa na shauku ya kuandika email
yako usiweke @ badala yake weka [at]. Kwa mfano badala ya kuandika
sikujui_Mkopachuma@yahoo.com andika
sikujui_Mkopachuma[at]yahoo.com.
Ni kwamba mtu mwenye akili zake ataelewa unamaana gani lakini wakati
kompyuta ina tafuta emails kwa kutumia kanuni hii
\b[A-Z0-9._%-]+@[A-Z0-9.-]+\.[A-Z]{2,4}\b haiwezi elewa, kwasababu @
haipo.


Kama wewe unapenda kuandika andika hovyo facebook na kama profile
yako iko wazi kwa search engine usishangae kupata spam...


Kwa wale wenye tovuti au wanaotaka kununua tuvuti nawashauri kuficha
taarifa ambazo hawata kuwa radhi kama zitakuwa mtandaoni. Naongelea
vitu kama jina, email na anwani za posta. Watumie ulinzi wa proxyserver,
kwasababu taarifa zote za anayemiliki tovuti huwa zipo whois kwahiyo
scraper inaweza ku-scrape whois database ili kupata taarifa wanazo zitaka.
 
Back
Top Bottom