Waliosoma zamani kabla ya kuwepo kwa auto-cards na arch-card softwares wamefanya kazi za Kihandisi kwenye mazingira magumu zaidi.
Imagine unapewa tender ya kudesign jengo la ghorofa 5 unajikuta unatumia muda mrefu kuweza kuikamilisha, Wakati kwa mazingira yetu ya Sasa nikikomaa ndani siku 2 hadi 3 nakuwa nimekamilisha kazi ya mteja.
Ninacho kumbuka Engineering drawing kutumia hizo device ilikuwa ni experience ngumu Sana hasa kwa tuliotoka form six Moja kwa Moja compared na waliosoma college kabla ya kuingia Chuo Kikuu.
Unakutana na Prof anakupa jengo la ghorofa kadhaa anakwambia umchoree right real, side view, aerial view n.k au unapewa object ana kwambia ichukue hiyo object ikate Kati alafu chora kitu unachokiona Ndani na ukute hujasoma technical drawing kama wenzako wa college au waliosoma Shule za Ufundi O'level 😢