Forbes: Floyd Mayweather ndio mwanamichezo tajiri zaidi duniani. Ampiku Messi na Ronaldo

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika porodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.

Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ua masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.

La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa.

Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema

Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12.

Mayweatjher ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m

"Mechi kubwa kati yake na McGregor 2017 iliwasaidia Mayweather na McGregor kujipatia pato la jumla ya $400m'' , alisema Kurt Badenhausen, Mhariri mkuu wa jarida wa Forbes Media.

"Lakini wachezaji wa mpira wa vikapu wametawala orodha ya wanamichezo 100 kufuatia kuongezwa kwa mishahara yao inayotokana na kandarasi ya maouyesho ya runinga ya $24bn

Aliongezea: "Orodha ya Forbes' ya wachezaji wanaopata mapato ya juu imejaa wanaume. lakini kumekuwa na mchezaji mmoja wa kike ambaye alifuzu baada ya orodha hiyo kuongezwa hadi majina 50 2010.

Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.

  1. Floyd Mayweather - Ndondi ($285m)
  2. Lionel Messi - Kandanda ($111m)
  3. Cristiano Ronaldo -Kandanda($108m)
  4. Conor McGregor - Karate, judo na Ndondi ($99m)
  5. Neymar - kandanda ($90m)
  6. LeBron James - Kikapu ($85,5m)
  7. Roger Federer - Tenisi ($77.2m)
  8. Stephen Curry - Kikapu ($76.9m)
  9. Matt Ryan - Soka ya Marekani ($67.3m)
  10. Matthew Stafford - Soka ya Marekani ($59.5m)
Tazama Orodha kamili

Marekani yatawala
Floyd Mayweather, Cristiano Ronaldo na Tiger Woods - wakiwa katika nambari 16 mwaka huu ndio wanamichezo watatu waliopo katika orodha ya wanamichezo tajiri zaidi ambao wamesalia katika orodha hiyo katika kipindi cha miaka 18 iliopita.

Mapato ya 2018 yalikuwa $22.9m, juu kutoka 1.5m mwaka uliopita kutokana na nyongeza ya mishahara miomgoni mwa wachezaji wa NBA.


Wanamichezo 11 kutoka michezo tofauti wameorodheshwa katika orodha hiyo na kutoka mataifa 22

Nyota wa ligi ya vikapu ya NBA wanaongoza katika orodha hiyo wakiwa wachezaji 40 miongoni mwa 100 tajiri.

Soka ya Marekani ndio mchezo wa pili uliowasilishwa sana ukiwa na wachezaji 18 , na kufuatiwa na mchezo wa baseball ukiwa na wachezaji 14 huku kandanda ikiwasilishwa na wachezaji 9 pekee.

Marekani ilitawala orodha hiyo ikiwa na wanariadha 66 huku Uingereza ikiwa na 5 wanaoongozwa na dereva wa F1 Lewis Hamilton katika nambari ya 12 na mapato ya $51m.

Mataifa ya Dominican na Uhispania yana wanariadha 3, hukiu Argentina, Brazil, Ufaransa, Japan na Venezuela wakiwa na wawili wawili.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hizo figures ni net au earnings kwa mwaka 2017 tu?
 
Top 20 ya kibongo mixer wasanii na wanamichezo

1* Platinumz
2* Sugu
3* kiba
4* pro Jay

Jazia na wewe
 
Then the writing is convoluted. Inaongelea wanamichezo tajiri zaidi wakati inataja earnings za 2017.

Inawezekana mtu kwa net wealth akawa wa 9 lakini kwa earnings za 2017 akawa wa 5. Vitu viwili tofauti.
 
[emoji818] [emoji818] [emoji818]
 
Hiyo namba 2 next year itashikwa na Zinedine Zidane kwa mkwanja atakaokua analipwa huko Qatar.
 
Mbwana Samatta ni namba ngapi ?
 
Mondi vipi tena hayupo??.....ok sorry ... sorry... sorry kumbe sio orodha ya wana muziki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…