Afrolink-Tz Consult Ltd
JF-Expert Member
- Feb 25, 2018
- 424
- 950
Habari zenu!
Leo katika jukwaa letu pendwa napenda tujifunze kitu kupitia kwa wenzetu ambao kwa namna moja au nyingine nao walipambana sana kufikia mafanikio fulani.
Makala hii nimeitoa ktk Jarida la Forbes chapisho la tarehe 01.07.2019 mwandishi ni Nate Huskins {Founder and President of Mashal Group LLC (exportusaautos.com), vehicles exporters from U.S and Canada}
Kupitia huyu jamaa kuna mambo 9 ambayo kwa yeyote akizingatia na kutekeleza uwezekano wa kufanikiwa na kufikia levo za juu ni mkubwa. Ni mambo ya kawaida sanaambayo si mageni kwa mimi na ww ila sema uzingatiaji wetu imekuwa changamoto. Mambo hayo ni
1. Kuweka juhudi katika utendaji
Hii ni changamoto ya kwanza kwa wajasiriamali na wanaotaka kuingia ktk ujasiriamali. Kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha muda kuwa mfupi sana ktk kazi zako. Jitahidi kufanyakazi zaidi ya muda wa kawaida, fanyakazi hadi muda wa ziada.
2. Upo tayari kupokea matokea yoyote
Je una moyo wa kupokea matokeo yoyote? Upo tayari kukabiliana na hatari zisizo mpangilio ie risk taker. Wengi wetu hatupo hatupo tayari kufeli na kujaribu tena na tena baada ya kufeli. Wengi wa waliofanikiwa walipita ktk mapito magumu ya kushindwa na kuendelea hadi kufanikiwa
3. Jifunze kukabiliana na watu wa aina zote
Kufikia mafanikio ni lazima ujifunze kukabiliana na watu wote pasina kujali wanaokupa changamoto na wanaokuunga mkono. Hii vilevile tambua unachokiamini wewe kwa sahihi sio wote wanakubaliana nalo. Je upo tayari kukubali kubadilka mtazamo iwapo haupo sahihi au utabaki na msimamo wako tu japo si sahihi?
4. Hakikisha unajiongezea utaalam na taaluma pasina kukoma
Kuongeza taaluma na utaalam si lazima mpaka uingia darasani bali jamii inayokuzunguka pamoja na wajasiriamali waliokutangulia ni somo tosha kwako. Ondoa aibu ya kuhitaji kuuliza na kujifunza kwa waliokutangulia. Hili jambo liwe lenye kuendelea na si kukomaa baada ya muda
5. Tumia mahusiano mema katika jamii kujijenga zaidi
Tambua kuwa mjasiriamali unahudumia jamii yote pasina kujali anaekuunga mkono na anaekukosoa. Tambua unajenga mtandao wa bidhaa zako kwa jamii. Hivyo jamii hii yote ni yako, ihudumie kwa usawa
6. Usiangalie nyuma
Jifunze kutoka kwa yaliyopita lakini isiwe kigezo cha kukufanya ubaki na kuegemea kwa mambo ya zamani.Epuka kuathiriwa na historia bali kila leo tengeneza historia mpya
7. Penda unayoyafanya
Siku zote kufanya jambo ambalo unalipenda zaidi na kuwa fursa huwa na matokeo mazuri sana. Hakikisha unapenda na kufanya kwa moyo mmoja ukiamini mafanikio kuapata kwa kiwango cha juu kabisa
8. Usiwaze sana juu ya mpango mbadala
Kuweka kipaumbele cha kuanzisha mpango mbadala kama utashindwa mpango wa kwanza hupunguza ufanisi wa utekelezaji wa mpango mkuu. ‘Focus’ katika mpango mkuu wa awali kana kwamba huna mpango mbadala ili usiathiri ufanisi na tija katika kutekeleza mpango mkuu
9. Usiendekeze mambo madogomadogo kuathiri maamuzi makuu
Kuna nyakati katika uwekezaji wowote kunamambo madogo madogo kwa namna moja au nyingine hujitokeza na kuona kama kikwazo kwako. Sio upuuzie lakini usitoe nafasi kubwa sana kuzuia maamuzi makubwa. Mfano, umeamua uzalishaji wa bidhaa lkn kuna changamoto za hapa na pale juu ya bidhaa, endelea kuzalisha bidhaa badala ya kusitisha uzalishaji
Haya ni mambo ya kawaida sana ambayo yapo katika mazingira yetu ya kiuwekezaji kwa nchi yetu ta Tanzania. Tunaweza kufanyia kazi kusonga mbele. Bila msimamo na maamuzi magumu hakika uwekezaji wowote ni mgumu na hakuna kulicho chepesi kukianza na hatimaye kufanikiwa. Tusilalamike sana, ni wakati wa kufanya maamuzi magumu sasa