Forbes lists 2013: Top 3....bill gates bado anaongoza na carlos slim hayupo tena kwenye top 3

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408
KWA MUJIBU WA FORBES MPAKA TAREHE 23 AUGUST LIST ILIKUWA KAMA IFUATAVYO

NAMBA 1: BILL GATES
Jamaa ameendelea kushikilia namba moja,nafasi ambayo aliipata mara ya kwanza tangu 1994. Na mwaka huu kiasi cha utajiri wake kimeongezeka kufikia dola bilioni 72 ukiachilia kiasi cha bilioni 28 alizotoa kusaidia jamii. Hapo ndio tunaona nguvu ya kutoa.(The power of giving).

NAMBA 2: WARREN BUFFET
Mzee huyu utajiri wake umeongezeka kufikia dola za marekani bilioni 58 licha ya matatizo ya kiafya aliyonayo. Na ikikumbukwa mzee huyu alitoa hisa zenye thamani kiasi cha bilioni 2 kwenda kusaidia jamii kupitia mfuko wa Bill and Melinda Gates. Na kiasi ambacho ametoa kusaidia jamii mpaka sasa ni dola bilioni 20. Na mwaka huu pekee kiwango cha ukuaji wa hisa katika kampuni yake ni asilimia 34. (The power of giving)

NAMBA 3: LARRY ELLISON
Utajiri wake sasa unafikia dola bilioni 41 na ni mmiliki mwenza na CEO wa Oracle corporation kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa software za kompyuta.
Na jamaa ametoa kusaidia jamii kiasi cha dola za marekani milioni 445. (The power of Giving).

TUKITAZAMA HAO MATAJIRI NAMBA MOJA MPAKA TATU TUTAONA KUWA WANATABIA YA KUSAIDIA JAMII KUPITIA KILE WANACHOKIPATA,HIYO NI MOJAWAPO YA NJIA AMBAYO INAWAWEZESHA KUENDELEA KUKUA KWA UTAJIRI WAO.
MFANO BILL GATES AMEENDELEA KUWA JUU KWA MIAKA MINGI MFULULIZO NA HATA UTAJIRI WAKE UNAENDELEA KUONGEZEKA KILA MWAKA LICHA YA KUENDELEA KUSAIDIA JAMII. MFANO TAASISI YAKE YA BILL AND MELINDA GATES INAFADHILI MIRADI MINGI SANA BARANI AFRIKA IKIWEMO TANZANIA.

**KUTOA SIO KWA TAJIRI TU BALI HATA MIMI NA WEWE TUNAPASWA KUTOA KILE TULICHONACHO KIWE KIDOGO AU KIKUBWA KUWASAIDIA WALE WASIONACHO**
 
aise mkuu kweli.mi nakuja kuwa kama hawa watu.angalia watoto yatima mtaani,watu wanaoangahika ada za kusomea,makahaba kwa ajili ya umaskini,wagonjwa wa magonjwa hatari yanayohitaji gharama wasizoweza afford,maskin wa kutupwa,waathirika wa midaharat.atleast kukiwa na mfuko wa watu kuchangia kwa ajili ya hawa direct si kisiasa. THE POWER OF GIVING,DO IT FOR THE GLORY OF GOD. nawakubali hawa jamaa
 


Anza na mimi...
 

ila hawa jamaa hawasemi wanatoa for the glory of God. Hata kanisani hawaendi kabisa. Wanatoa ili watu wawe na maisha bora zaidi. Wengine kama Ted Turner aliye toa bilioni 10 za marekani wanasema hakuna Mungu. Wengi wetu tanatoa ili Mungu atubariki, nadhani kutoa kwa design hiyo ni kama kujaribu ku manipulate Mungu ili tuongeze mali.
Mungu ameshatustukia
 

mi napenda kufanya si kwa sababu,ila inaniumiza mwenyewe tu coz nmeshawah onja ugumu.nazan mi ntafanza sababu wote ni watu wa mungu tuna haki ya kuishi kistarehe na furaha.kweli wengi ni matajiri wa amerika ni maatheist na wengne wanadini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…