Foreign meddling: Raila na siasa za Zimbabwe

Kafrican

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
7,251
Reaction score
7,037
Juzi juzi chama cha ODM kilichukua msimamo rasmi na kutangaza kwamba kinasikitishwa na matukio yaliofanyika Uganda kwa mwanasiasa Bobi Wine.
Sasa kuna hii habari iliotokea inayosema Raila amehusika kuwapa mawaidha chama cha upinzani cha Zimbabwe ili kisumbue serekali mpya ya zimbabwe hadi wapewe kiti kwenye meza.
The same same Raila wakati ule wa Uchaguzi mkuu wa Kenya aliambia nchi za Magaribi zisitubuthu kuingilia kati Sisa za Kenya kwa kuchukua msimamo flani.... mbona tunafanyia wenzetu jambo ambalo hatutaki kufanyiwa jameni.... Nchi za magaribi zikifanya hivi, inaitwa "foreign interference/meddling", nchi za Africa zikifanya hivyo hivyo, inaitwa "helping our brothers and sisters"...

Kila nchi iwachwe itatue shida zake ndani kwa ndani. Jirani hawezi tatua shida za we na bibi yako, na hata akitatua kwa leo, kesho atawapata mnagombana tena.
Maybe wakati ule wa 2007 PEV tungeachiwa tuendelee kupigana hadi tuamue wenyewe imetosha, tukae chini wenyewe kwa wenyewe na tutatue shida na tofauti zetu, leo hii labda hatungekua na uchumi huu tulio nao lakini tungekua tulitatua shida za ukabila once and for all. lakini vile akina condoliza rice na Kofi annan walituketisha chini, by 2017 election ilikua tumerudi pale pale!!!!


Soma hapa jinsi siasa za Raila zinatumika na chama cha upinzania Zimbabwe. Chamisa copies the Kenyan playbook
 
Mwisho wa siku huo upinzani wa Zimbabwe utajuta sana kutumia ushauri wa Raila. Kuna jamaa fulani kutoka nchi jirani alimuunga mkono Raila uchaguzi uliopita huku Kenya akaangukia pua na kubaki na maumivu ambayo hayajatulia hadi sasa hivi.
 
Mwisho wa siku huo upinzani wa Zimbabwe utajuta sana kutumia ushauri wa Raila. Kuna jamaa fulani kutoka nchi jirani alimuunga mkono Raila uchaguzi uliopita huku Kenya akaangukia pua na kubaki na maumivu ambayo hayajatulia hadi sasa hivi.
Akili yako ni ndogo, hakuna mtu aliyeingilia uchaguzi wenu wala hakuna support yoyote Raila aliyoipata kutoka Tz, ni media zenu zinatengeneza habari halafu mnajikenya wenyewe.
 
Akili yako ni ndogo, hakuna mtu aliyeingilia uchaguzi wenu wala hakuna support yoyote Raila aliyoipata kutoka Tz, ni media zenu zinatengeneza habari halafu mnajikenya wenyewe.
Tz? Nilikuwa naongea kuhusu rais Farmajo wa Somalia. [emoji1]
 
Naomba kukinzana na maini yako, ifahamike ugomvi wako na mkeo sitaingilia wala kujali sana, ila ukipitiliza kwa mfano unyanyue upanga dhidi yake, hapo tegemea kipodo cha majirani.
Leo hii Kenya ndio kaka mkubwa ukanda huu, na ndio unaona hata juzi nchi yetu ilimlinda yule Tundu Lissu wa Tanzania na kumhakikishia usalama muda wote hadi akaondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…