Forever Living na Biashara ya soko la kimtandao Untold Facts

Msamiati

R I P
Joined
Mar 6, 2011
Posts
1,063
Reaction score
700
Kwanza kabisa napenda niweke wazi kuwamimi sina uwanachama hai wa kampuni yoyote ya inayofanya biashara yasoko la kimtandao kwa hivi sasa, na sina masilai ya aina yoyotekutoka kwenye biashara hii zaidi sana Nimeamua kuandika Makala hiikuhusiana na biashara ya soko la kimtandao kutokana na mkanganyikomkubwa ambao umekuwepo miongoni mwa watu wanaoisikia biashara hii kwamara ya kwanza na hata wale walioingia kwenye biashara hii siku zahivi karibuni nimeandika nikiwa na nia kubwa kabisa ya kuwapa ufahamumzuri kuhusiana na kile mlichoamua kukifanya.


Mimi nimeshawahi kuwa katika industryhii kwa zaidi ya miaka miwili kabla ya kuamua kupumzika mapema mwaka2012. Katika kipindi cha miaka miwili niliyoitumikia biashara hiikupitia kampuni ya ForeverLiving, nimefanikiwa kujifunza na kuielewavizuri sana biashara ya soko la kimtandao na ufanyaji wake.


Na katika kukudhihirisha tu umahiriniliokuwa nao na ufahamu mzuri katika biashara, ndani ya kipindi chamiaka miwili niliyofanya hii biashara nilifanikiwa kupata ngazi yakutambulika inayoitwa Supervisor. Hivyo basi, nikutoe shaka nakukuhakikishia kuwa nitaenda kukwambia kitu ninachokijua na ambachonina uhakika nacho.


Sehemu kubwa ya safari yangu kamamfanya biashara wa biashara ya soko la kimtandao niliitumia kujifunzana kusoma vitabu mbali mbali hususan vitabu vya mfumo wa masoko(Marketing plan), Sera za kampuni(Company Policy) na historia yabiashara yenyewe kawa ujumla.


Nitakacho jaribu kufanya katika makalahii ni kukwambia vitu vyote ambavyo mara nyingi huwa havisemwi kabisaau havizungumziwi kwa uwazi kwenye mikutano ya Fulsa za kibiasharaalmaarufu kama BOM. Nia sio kukutia hofu ya kuifanya hii biashara aukukukatisha tamaa kama ulisha ianza, bali ni kukujenga na kukupamaamuzi sahihi kwani mimi mwenyewe ni kati ya watu tuliogundua sirikubwa ya mafanikio iliyopo ndani ya mfumo huu wa kibiashara.


Kwa maelezo hayo basi, ili uwezekufaidika zaidi na makala yangu ni vema ukawa tayari umesha hudhuriamkutano wowote wa Fursa ya Biashara (Bussiness Oportunity Meeting).Kama ndio unasikia kuhusu biashara hii kwa mara ya kwanza tafutamtaalamu yoyote anayefanya biashara hii ili aweze kukupa maelekezobinafsi (One to One Training), Hata kama huna shida ya kufanyabiashara hizi, mimi binafsi huwa narecomend mafunzo hayo kwaniyatakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine ukiwa kama mtuunayetafuta mafanikio katika maisha.


Ukihitaji msaada wa kuwapata watu haounaweza kufika kwenye vituo vyao vya mafunzo Ambavyo vipo katikamikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam. Au kwa msaada zaidiunaweza kuwasiliana na Mr Seth Saimon Mwakitalu ambaye mimi naaminini moja kati ya wakufunzi mahiri sana wa biashara ya soko lakimtandao, mzee huyu unaweza kumpata kwa kumuulizia kwenye makaomakuu ya kampuni ya FLP Tanzania yaliyopo Pugu road Dar es salaam.


Kama umeshapata training au maelekezohayo you are ready to go...


Biashara ya Soko la kimtandao ninini ?


Kitu ambacho inawezekana hukuambiwakuhusiana na biashara ya soko la kimtandao ni ukweli kwamba, hii nibiashara inayohusiana na mambo mawili, kwanza ni kuwa mteja nambamoja wa bidhaa za kampuni pili ni kutafuta wateja wapya. Shughulizote utakazokuwa ukizifanya, mafanikio yote unayoambiwa utayapatayanabebwa na vitu viwili tu, na hivi sio ombi ni lazima ili uwemfanya biashara, kwanza lazima utumie pili lazima ushawishi watuwapya kuwa wateja.


Biashara ya soko la kimtandao sio yakila mtu


Katika sehemu mbili nilizo zielezanimetaja Kutumia na kuleta wateja wapya. Kwenye kuleta wateja wapyakampuni imezuia kabisa kutanfaza bidhaa zake kupitia media, mabangoau kuweka bidhaa kwenye duka au sehemu ya wazi ya matangazo auminada.

pitia kitabu cha sera za kampuni kipengele cha 16 kwenye kurasa ya 25. Soma kifungu cha 16.02 h


Sheria hii ili lenga kuhakikisha bidhaazinatangazwa kwa njia ya kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwinginehivyo kuweka fulsa kwa kila mmoja kuwa na uwezo wa kupata watu wapyawa kutumia bidhaa kwa uwiano ulio sawa.


Sheria hii imevunjwa kabisa nakupelekea biashara hii kuwapa nguvu zaidi watu wenye uwezo wakujitangaza na wamiliki wa maduka na maeneo ya biashara. Hii imeondoafulsa nzuri ya kibiashara ambayo hapo awali ilikuwepo kwa watu wakipato cha chini kabisa. Sasa hivi mazingira mazuri ya kibiasharayapo kwa baadhi ya watu tu na si kwa kila mmoja.


Bidhaa za Kampuni sio dawa


Bidhaa za kampunisio dawa wala hazina uhakika wa asilimia 100 wa kutibu maradhi.Bidhaa hizi zipo 100% kwaajili ya afya bora na 50% kwa ajili yamaradhi, endapo zingekuwa na hata 75% ya kuondoa maradhi basizingeitwa dawa bila shaka.


Ngoja nisimamekidogo then nitaendelea ….
 
Mkuu tiririka kama maji ya dawasco. Tupe hizo facts
 
tupe habari maana mm kuna mtu anataka kuniingiza huko toka feb 14 hadi leo hachoki kunishawishi
 
tupe habari maana mm kuna mtu anataka kuniingiza huko toka feb 14 hadi leo hajachoka kunishawishi hadi ss hivi jikiona simu yake sipokei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…