Nataka kujiunga na Forever Living products niwe nauza bidhaa zao za alovera kama nyia ya kuongeza kipato changu.wenye uzoefu naombeni ushauri au wale mliojiunga na mko mpaka sasa au mliojitoa ningependa maoni yenu.Je inalipa kweli?
Usiwe mjinga ndugu si kila jambo unatakiwa kuomba ushauri wa aina hii hayo ni maisha yako yashike. Omba ushauri kwa waliondani ya forever sio walio nje sawa. Ukitaka kujua utamu wa ndoa usiende kwa msela nenda kwa mwana ndoa.
Hii ni biashara ambayo u need sales skills kiuhakika na ili uone faida lazima uuze vitu vingi. Kwanza utapewa maneno mengi mazuuuuriii ila ingia uone ngoma yake sasa. Walioingia mwanzo wanafaidi sana so if you can build ur network go ahead.
Kitu kingine angalia wanaokuzunguka Je wanaweza kununua products? maana nina bei sana mf dawa ya meno ni > 10,000 wakati colgate herbal ni 3000 au the famous sensodyne inayoaminika ni 8000. Analyse ipasavyo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.