Hii biashara kweli ipo, kwani bureau de change si wanafanya biashara ya kuuza hela? biashara zote duniani kati ya nchi na nchi zinategemea kubadilisha thamani ya fedha kutoka nchi moja kwenda thamani ya fedha ya nchi tofauti ingawa kwa kiasi kikubwa ni fedha ya Marekani, Ulaya na Japan ndizo zinatumika zaidi.
Hii ya mtu mmoja mmoja kuwekeza kwenye forex kupitia kwa broker basically ni kumkusanyia mtaji yeye ili anapouza mnagawana faida. Na faida utapata kama bei ya kununulia itakuwa chini ya ile ya kuuzia, vinginevyo utakula hasara. Sasa kwa vile masoko ya fedha yako dynamic sana kutegemea na siasa/uchumi na uhusiano wa kimataifa ndo unaona forex trader wengi wanakuwa bize kufuatilia mwenendo wa masoko ya fedha, habari za biashara na hata siasa duniani.
Sasa basi kama zilivyo biashara nyingine zozote hata hapa kwenye forex kuna wajanja ambao kazi yao ni kuwaingiza mjini watu wasio na uelewa wa namna biashara inavyoendeshwa. Kifupi matapeli wapo kwenye kila aina ya baishara.
Unachopaswa kufanya ni kuwa makini na kujifunza sana ili uweze kushiriki kwenye hii biashara.
Kumbuka kitu kimoja though, Forex ni very risky business and that is why it has good returns, ila ukila hasara ni hasara ya maana.
kazi kwako sasa![/QUOTE
Bureau de change wanatengeneza faida at the expense ya yule anayehitaji pesa ya aina Fulani sasa je hii forex yenyewe unatengenezaje pesa, ungetoa tu maelezo mafupi tu kwamba ni either unanunua na kuuza au kuna kuhold iyo currency au inakuaje kuaje hii. Hii biashara ya kubadilisha fedha ipo na mabenki wanapiga sana hela ndo biashara yao hii na wanatengeneza pesa at the expense ya wafanyabiahara wanao fanya biz za import and export lakini kibongo bongo hii forex yenu ni scam and some sort of multi level marketing na mnachofanya nyinyi na huyo ticha wenu si jambo la kiungwana kuna watu washaanza kuwa frustrated wameanza kuona mauza uza kwenye hii biashara yenu.