Mtaalam_the_first
Member
- Sep 8, 2016
- 41
- 91
Habari,
Ndugu Watanzania, mimi nikiwa kama mdau ya Forex Trading, nimeona kuna ulazima wa kuandika Makala hii kumsaidia Mtazania yoyote uko nje atakae au anaye tamani kujiingiza kwenye hii biashara. Waweza jiuliza kwa nini nachukua jukumu hili, mafanikio katika sekta hii sio rahisi kama inavyo onekana kwenye mitandao na vyombo vya habari. Safari yangu haikua rahisi, ilikua ni safari ya milima na mabonde, yaliopelekea matizo chungu nzima ambayo haina maana ya kuyaweka hapa, zaidi ya ambacho nataka ukifahamu.
Hivyo basi nimeona nifanye hivi kama njia moja wapo yakurudisha au kutoa kwa jamii bure kabisa kumsaidia yule anaeanza au mdau wa biashara ya online forex trading, ili kuepukana na matatizo makubwa niliyo yapitia na kumsaidia kusogea kimafanikio kwa urahisi zaidi.
Kama ningekua na mashine ya kurudisha muda nyuma, niwe mimi yule mgeni wa forex trading, ningefanya hivyo ili tuu niwe na haya ninayo yafahamu leo hakika ningefanya mambo yawe rahisi zaidi kwangu. Lakini kibaya ni kwamba hakuna mashine kama hiyo lakini kwa wewe unaenza sasa hii nikama lulu kwako hivyo basi haya ndiyo mambo ambavyo ningeyajua mwanzoni naamini kwa asilimia mia moja mambo yangekua kitonga.
NI VYEMA KUZINGATIA USIMAMIZI MZURI WA MTAJI KULIKO JAMBO LOLOTE LINGINE.
Tunapoanza Biashara ya trading, tena haswa trading forex wengi huja na ndoto mbali mbali na taswira binafsi yakujitajirisha haraka. Lakini uhalisia ni kwamba njia pekee yakujitajirisha ni kuwa makini na jinsi unavyo risk pesa zako sokoni kwenye kila trade unayochukua.. Mfano, unaanza na mtaji wa $1000 sitegemei kukuona unarisk kwenye trade yoyote zaidi ya 2% ya mtaji wako ambayo ni $20. Kwa ambao wataanza na mtaji chini ya $300 ningeshauri kufungua cent account ilikukuwezesha kufanya usimamizi wa mtaji wako vizuri. Ukizingatia upande wa hasara basi upande wa faida kamwe hautokua na shida. kwenye kila trade unayochukua hakikisha unapata faida ya zaidi ya kile kiasi ambacho hua una risk kwa lugha ya kitaalam tunasema RISK TO REWARD. Maanake yake faida zako ziwe Mara mbili na zaidia ya kiasi chako cha risk.
EPUKANA NA WAZIMA NDOTO
kuna msemo unasema "WEWE NI WASTANI WA WATU WATANO WANAOKUZUNGUKA" sasa kama watu watano wanaokuzunguka hawaamini unachokifanya lazima utakwama tu. Hivyo nakushauri tafuta na jenga uhusiano na watu wanaoamini na kupigania unachokipigania mta saidiana kufika mbali haraka zaidi. Hata kipindi cha mambo yanapokua magumu mtashauriana na kutiana moyo.
NI RAHISI KU OVERTRADE KULIKO UNAVYO FIKIRIA.
Kitu ambacho niligundua baada ya kuwa mzoefu kwenye biashara hii siku za mwanzoni nilikua na overtrade na hata siku gundua na fanya hilo.
Nirahisi kutafuta visingizio vya trades unazochukua kwa wingi (kwaku overtrade). Lakini jibu kamili nikwamba je ime timiza vigezo vyako vya kutrade yaani (strategy)
Overtading nikitendo cha kuchukua trade nje ya strategy yako na niamini mimi, sio jambo gumu sana kufanya kwenye hii biashara, haswa kwa Traders wageni na nijambo ambalo lina umiza sana na kurudisha nyuma hatua zako zakimafanikio
MATUMIZI YA TIMEFRAME NDOGO NI HATARI
Ukiangalia kwa makini hizi points zote zinaingiliana kwa mfano overtrading inasababishwa nakuangalia timeframe ndogo kama zile chini ya ‘1HOUR’, laiti kama ningerudi nyuma kipindi nikiwa mgeni na forex ningejieleza haswaa umuhimu wa matumizi ya timeframe za juu. Matumizi ya timeframe za chini yatakupelekea kuovertrade kwa sababu utahisi unaona fursa nyingi sokoni wakati kiukweli izo ni kele tu za soko. Kirahisi ni kwamba fursa zinazo patika timeframe za juu zina Asimilia kubwaa Zaidi ya kukutengenezea faida kuliko zile zinazo patikana timeframe za chini.
HUWEZI KUZUIA HASARA KABISA.
Inafurahisha sana unakuta traders wengi wanahangaika kuzuia hasara wakati ni jambo ambalo haliwezekani kuzuia hasara kabisa bali unaweza tu kuzipunguza kwa kufuata “system” yako.
Kama unafanya mambo kama haya: trading bila stoploss, kusogeza stoploss kwenda breakeven mapema sana, kuchukua faida ndogo ndogo kulinganisha na hasara zako yaani kwa kifupi ni unajaribu kuepusha hasara na hicho nikitu kibaya rafiki yangu.
ZINGATIA KWENYE KUJIFUNZA NASIO KUTENGENEZA FAIDA UNAPOANZA TRADING.
Huwezi kufanikiwa na trading kama unachokiwaza ni faida tu na ndoto zisizo madhubuti. Kuwa Trader mzuri ndo kitu kinachotengeneza pesa sokoni na sio vinginevyo, mafanikio katika trading yanatokana na kua mjuzi na mzoefu wa ‘system’ yako na pia kua mzoefu na tabia yako ilivyo pale unapofanya maamuzi sokoni. Hivyo basi utaweza kufanya haya kwa kuzingatia kujifunza nasio kutengeneza faida na pia kuipenda kazi yako kwa kufanya mazoezi kama ‘backtesting’ n.k
Haya ndo machache Ambayo mtu yoyote akiyazingatia uko nje atafanikiwa na Trading. Ningependa kumuamsha mtu yoyote atake jiingiza kwenye biashara hii kuichukulia kwa uzito na umakini kama kazi nyingine yoyote nasio kama Kamari yakukutajirisha haraka sana bila jitahada zozote.
FOREX TRADING Inawezekana!!