Form 4 mwenye ndoto za kusomea IT usipoteze mda wako kwenda form 6, nimekupa ramani nzima hapa

Kuna baadhi ya kada 5 & 6 haina umuhimu sana kwao mojawapo ni hii IT.

Ila hapo kwenye vyuo mkuu, haya masuala ya IT kua vyema kichwani ndio cha muhimu haijalishi umesoma UDSM au chuo gani cha muhimu tu kiwe kinatambulika kiserikali.

IT inahitaji hasa ujuzi wako tofauti na kada nyingine ambazo ni rahisi kucopy toka kwa wafanyakazi wenzio na ww ukaishi umo umo. Ila hii utastukiwa tu na kuonekana kilaza hata mtaani utapaona pagumu sana.
 
Sidhan kama case hiyo ni valid kwa sasa. Naona ajira zinatolewa kwa wote. Ukipata usaili unapita haijalishi chuo gani
Watu wanakalili sana mkuu. Ndio chanzo cha wahitimu wa kidato cha sita kukimbilia UDSM kwa wingi na kwenye course za ajabu ajabu tu kwa kua kaka/dada zao wamewaambia ukisoma UDSM ni rahisi kupata ajira.

Hii kitu imepungua kaa kiasi kikubwa sana siku hizi. Tena kwa hizi course zinazohitaji ujuzi zaidi hii imekua ni nadra sana kutokea.
 
Nako huko india kunategemeana na chuo ulichoenda kusoma pamoja na bidii yako, kuna vyuo huko india havitambuliki hata na TCU, ukimaliza huko hicho cheti huwezi tumia huku kuombea ajira

Kwa faida ya wengine, unajuaje list ya vyuo vinavyotambuliwa na TCU vilivyopo nchi za wenzetu...?

Swali jingine ni kuhusu hizi online courses, unaposoma online kwa mfano Udemy au Coursera then ukapata cheti, hiko cheti kinafaa kuombea Ajira...? Au kinahitajika upeleke TCU for verification mkuu...?
 
1.Kujua vyuo vya nchi fulani kama vinatambuliwa na TCU, Ingia kwenye tovuti za TCU na NACTE soma vigezo na masharti husika.

2.Cheti cha kozi za online nacho ni lazima kiwe verified by TCU/NACTE.

3.Ndiyo, Unatumia kuombea ajira kama ukihitaji kufanya hivyo.
 
Cheti cha darasa la saba nacho huna?
Kama unacho nenda chuo cha mafunzo ya ufundi yaani VETA,
Uwaonyeshe cheti na uwaambie kozi zote ulizopiga mtaani na una ujuzi nazo,
Watakupa mtihani wa vitendo wa kozi husika ukifuzu utapewa cheti.

Kila kozi ina gharama yake.

Nafikiri utapewa mtihani wa vitendo kwa kozi mbili ili upate hiyo yenye sifa ya cheti cha form four yaani NTA LEVEL 4.
 
Chet cha form four ninacho na nilifaulu kwenda A- level but sikwenda kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu,
 
Chet cha form four ninacho na nilifaulu kwenda A- level but sikwenda kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu,
Hongera.
Sijajua unakwama wapi mkuu wangu wakati una cheti tena chenye ufaulu mzuri wa kwenda A-Level?
Sijui kama unataka kujiajiri au unataka kuendelea na masomo. Maana nilitaka kukushauri kwa kutumia cheti cha four unapiga kozi ya NTA Level 5/6 pale VETA badala ya kwenda A-Level halafu una-apply kwenda Chuo Kikuu katika vyuo vya serikali na utakuwa na uwezo wa kuomba mkopo chuoni hapo. Gharama ya kozi pale VETA inategemeana na kozi unayoichukua lakini zipo za kuanzia 200K, 250K, 300K, 350K, 450K, N.K
 
Chet cha form four ninacho na nilifaulu kwenda A- level but sikwenda kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu,
Kuna njia nyingine huwa inatolewa na Serikali kwa mtu ambaye alifaulu form four ama alipata D4 ya ufaulu halafu hakuendelea na masomo ya A-Level.
Kipindi kile ilikuwa unatoa shilingi laki nne [400,000=TSH] kwenye shule ya Serikali yenye masomo ya A-Level halafu wanakuunga kwenye mfumo kusoma saa 8 mchana - saa 12 jioni ukipiga double masomo ya 5 na 6 one year halafu matokeo yakitoka ukafaulu unaenda chuo kikuu na una apply mkopo.
 
Asante kwa ushauri wako
 
Nitaufanyia kazi mkuu
 
hii nchi ndio maana tunazidi kudidimiana kutengeneza vijana wa hovyo, acheni kuwapotosha vijana wa watu na shortcut zenu zaa maisha, waacheni waende advance, kunafaida nyingi atapata kuliko kupitia vishortcut, afadhali aende advance then aje kuanzia diploma ,then degree na ngazi nyingine atajenga career yake vizuri, atapata exposure na experience, na masomo kama hesabu hayatampa stress. pili, acha kushauri watu wasome ili aje waajiriwe, course kama I.t ni moja ya course amabazo ukikomaa na skill fulani ulioichakgua, utaweza kujiajiri mwenyewe .
 
Mdog wangu alipata D 5 form 4 nkampeleka certificate ya IT, akaunga Diploma.. akatapa kazi ya uhakika wizara flan.. kapangiwa dsm na kajisomesha degree sa hv anafanya Masters!
Tena Boss na anakaa nyumba ya wizara Mbezi beach
 
Hii mada ni ya siku nyingi ila nimevutiwa na kipengele kimoja hapa ndugu mwandishi kama bado upo hai naomba ufafanuzi zaidi au kama kuna mdau anajua pia atupe mawili matatu.


SWALI JE! HII MITIHANI YA SAT TEST ILI UPATE UFADHILI INAHUSIANA NA KUTESTIWA KWA UELEWA WA LUGHA AU INABASE KWENYE MASWALI GANI HASWA NA JE UKIPATIWA UFADHILI UNACHAGUA CHUO CHA KWENDA KUSOMA MWENYEWE AU NDIO HATA WAKIKUPANGA AFAGHANISTAN UENDE TU?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ