KWELI Fr. Elipidius Rwegoshora, ambaye ni Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Asimwe Novath, ni Padri katika Jimbo la Bukoba

KWELI Fr. Elipidius Rwegoshora, ambaye ni Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Asimwe Novath, ni Padri katika Jimbo la Bukoba

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Msemaji wa jeshi la polisi kasema ni padri, watu wanatwambia ni mlevi mmoja hivi.

Which is which??

1718972666552.png
 
Tunachokijua
Parokia ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa Kanisa Katoliki, Parokia hufuata baada ya jimbo (dayosisi) hufanyika uchungaji wa kila siku chini ya kasisi(Padri/Paroko) anayemwakilisha Askofu.

Paroko ni padri aliyekabidhiwa na Askofu uchungaji wa parokia, ambayo ni sehemu ya jimbo.

308514787_403267711969923_6807116195680634787_n.jpg
Mei 30 2024 liliripotiwa tukio la kupotea kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Asimwe Novath, ambapo jitihada mbalimali za kumtafuta ziliendelea kufanya na watu wakiwemo Jeshi la Polisi, Lakini Juni 17 2024 Mwili wa mtoto huyo ulipatikana ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo.

Mnamo 19 Juni 2024 Jeshi la Polis lilitoa Taarifa ya kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya mtoto Asimwe Novath, miongoni mwa waliokamtwa ni Baba mzazi wa Asimwe na Elipidius Rwegoshora ambapo Kwenye Barua ya polisi walimtaja kama Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika.

Kutwaja Paroko Msaidizi katika orodha ya watuhumiwa wa mauaji kumeibua hisia tofauti mitandaoni, Watu wengi wakihitaji kujua iwapo ni Paroko kweli au lah, huku wapo wanaodai alikuwa Padri lakini alifukuzwa kwa utovu wa nidhamu lakini wapo wanaodai alirudishwa.

Je, ukweli ni Upi?
JamiiCheck
imepitia taarifa mbalimbali na kubaini kuwa jina la Elipidius Rwegoshora (tazama) lipo katika orodha ya Mapadri wa Bukoba. Tazama hapa Chini:

1718928497388-png.3021870

Pia, JamiiCheck imepitia Tovuti ya Jimbo la Bukoba na kukuta jina la Elipidius Rwegoshora kuwa mmoja wa Mapadri waliopo katika orodha hiyo (Tazama)

1718912708608-png.3021791

Askofu wa Jimbo la Bukoba, Mwashamu Jovitus Mwijage, kupitia gazeti la Mwananchi la 19 Juni 2024 amethibitisha kuwa Mtuhumiwa wa mauaji ya Mtoto Asimwe, Elipidius Rwegoshora, ni Padri na alikuwa akitoa huduma za Kichungaji katika Jimbo la Bukoba.

"Tunahuzunishwa sana na taarufa ya mauaji ya mtoto Asimwe, kwani sisi kama kanisa Katoliki ni Walinzi wa kwanza wa uhai wa Mwanadamu, Tunaiombea familia yake na kuiombea roho yake ipate pumziko la Amani Mbinguni.

Hata hivyo tumesikia taarifa ya watuhumiwa mmojawapo akiwa Padri Rwegoshora. Ni kweli Padri huyo ni wa Jimbo Katoliki Bukoba na tumechukua uamuzi wa kumsimamisha kutoa huduma zote za kichungaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya Sheria.

Baada ya vyombo vya kisheria kumaliza kazi yake ndipo taratibu nyingine za Kanisa Zitafuata". Ameeleza Askofu Mwijage

1718970631323-png.3022198

1718970719127-png.3022199
Pia, Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Samuel Muchunguzi alithibitisha kuwa kama kanisa walikuwa na mtu mwenye jina kama hilo la Elipidius Rwegoshora japo hakuwa na hakika kama aliyekatwa ndiye kwa kuwa hakuhusishwa na Jeshi la polisi katika hatua za kukamatwa kwa mtuhumiwa na kwamba huenda akawa siye au ndiye kwa kuwa majina huweza kufanana.

Alisema atafutwe Askofu Mkuu ambaye atazungumzia suala hilo, Msaidizi huyo wa Askofu amelaani kitendo hicho cha kinyama alichofanyiwa Mtoto Asimwe na kusema wao kama kanisa hawaungi mkono na wako kwa ajili ya kulinda uhai wa mwanadamu kwa kuwa una thamani kubwa.

JamiiCheck imethibitisha kuwa mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya mtoto Asimwe, Elipidius Rwegoshora, ni Padri katika jimbo la Bukoba ambaye amesimamishwa kutoa huduma za uchungaji mara baada ya kupatikana na tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya Mtoto Asimwe.
Msituchoshe kwani dini imesema ukikosea tukutetea kwa nguvu kama ni kwel hukum yake ipo kama uongo fresh yaani watu humu unaona wanasimam kutetea
 
Msituchoshe kwani dini imesema ukikosea tukutetea kwa nguvu kama ni kwel hukum yake ipo kama uongo fresh yaani watu humu unaona wanasimam kutetea
Sawa, lakini ukweli wa taarifa ni muhimu kuondoa sintofahamu
 
Back
Top Bottom