Mkuu Waka,
Kuna watu nafahamu wametajirika na wengine wamefilisika. Na kama kila aina ya biashara. Inategemea matangazo yako, eneo lilipo duka, bei zako, muuzaji yuko sharp kiasi gani nk. Ni kama hotel zipo eneo moja, moja nzuri na haina watu na nyingine ya kawaida ila ina watu wengi tu wamekaa.
Mie nauza jumla kwa bei nafuu sana ukilinganisha na ubora. Unaweza kuchukua kadhaa na nikakupa na Tester ili watu wajaribu. Kama unauza nguo au vitu vinavyofanana na hivyo, unaweza kuwa nazo chupa kadhaa na ukawa unauza. Ila kwa mfano unauza mbao au cement na ndani unaweka perfume basi itakuwa ni shida sana. Si mbaya kama unauza vyakula maana inaweza kuwa mtu kaja kununua unga na sabuni na ghafla anaona perfume au vipodozi vingine.
Nafikiri inalipa kwani kwa sasa kuna Order kadhaa zimeshawekwa kiasi kwamba mzigo ukifika tu, watu wanachukua. Mzigo ukifika basi ntakujulisha na uende kuziangalia. Ila bei zetu kwa jumla Max kwa chupa moja ni Tsh.20,000 na huenda zikapanda hadi Tsh25,000. Nyingine zote ni chini ya hapo. Ila nina uhakika wengi wanauza kwa rejareja hadi Tsh.40,000/ kwa chupa au hata zaidi maana sijui wanauzaje kwenye maduka yao. Wengine wananunua na kuuza mashuleni au ofisini.
Zangu si bei nafuu kama za Kichina ila pia si bei mbaya kama zinazouzwa laki moja kwenda juu. Quality yake zinakaribia sana hizo za bei mbaya ila kwenye bei ni nafuu mno kwa sasa maana tuko kwenye Promotion. Huko mbeleni zinaweza kupanda kidogo bei hasa kiwandani wakianza kuniuzia kwa bei ya kawaida maana sasa hivi wamenipa Discount kubwa na mie naitumia kwa kuuza bei nafuu. Wengi wakitumia asubuhi, wanashinda na manukato siku nzima na hata wakioga bado inabaki kwa mbali.
Karibu uanze kwa chupa kadhaa na utaona kama inalipa au hailipi.