thesym
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 3,843
- 4,796
Hizi timu mbili Ufaransa na Uhispania zilikuwa ni mabingwa watetezi wa kombe la dunia kwa miaka husika lakini kila kikosi kilikuwa ni kibovu.
Watu wengi kipindi hiko walidhani hizo timu zingetetea ubingwa kulingana ukubwa wa majina wa wachezaji.
Lakini mwisho siku kilichotokea ni kinyume chake.
Ufaransa ya mwaka 2002 na Hispania ya mwaka 2014 zilishindwa kuvuka hatua za makundi.
Hata kabla ya kufikiria matokeo ya mechi walizocheza hebu kione hiki kikosi cha Ufaransa mwaka 2002.
Zidane yupo nje anauguza majeruhi, ufaransa inaundwa wafungaji bora wa ligi tatu tofauti.
Katika msimu wa mwaka 2001/2002 hawa wachezaji watatu wa Ufaransa waliongoza kwa ufungaji katika ligi za Ufaransa, Uingereza na Italia.
Lakini amini usiamini Ufaransa hii haikushinda mechi hata moja wala kufunga hata goli moja.
Kwani matokeo ya ufaransa iliyokuwa kundi A yalikuwa ni mabaya mno.
Ufaransa kombe la dunia la 2002 Walicheza mechi tatu, walitoa suruhu ya bila kufungana mechi moja na zilizobaki walifungwa.
Haya ndio matokeo ya kikosi kibovu cha ufaransa 2002 yalivyokuwa.
Mechi ya kwanza juni 1 2002: Ufaransa 0 vs Senegal 1
Mfungaji wa goli la Senegal: Papa Bouba Diop.
Mechi ya Pili juni 6, 2002: Ufaransa 0 vs Uruguay 0
Mechi ya tatu juni 11,2002: Denmark 2 vs Ufaransa 0
Wafungaji wa magoli ya Denmark: Dennis Rommedahl na Jon Dahl Tomasson.
Hata ukiangalia vilabu ambavyo wachezaji wa ufaransa walivyokuwa wanachezea unashindwa kuelewa jinsi gani kocha wa Ufaransa ya 2002, Roger Lemerre ambaye baadae alihamia Tunisia alishindwa kuunda timu bora yenye ushindani.
Kocha wa Ufaransa 2002, Lemerre.
Kikosi kingine kibovu cha bingwa mtetezi ni cha hispania cha mwaka 2014, mashindano ambayo yalifanyika brazil.
Japokuwa anguko la Hispania lilianza kuonekana kwenye fainali ya kombe la mabara la 2013.
Ambapo walifungwa magoli matatu kwa bila na Brazil.
Lakini kwa kikosi kilichopo kwenye hii picha, ni ngumu kuamini kuwa hiki kikosi kilifungwa jumla ya mabao saba na kipigo cha kudharirika toka kwa Uholanzi.
Hispania ilicheza mchezo wake wa kwanza kwenye kundi B na Uholanzi, kisha wakacheza Chile na wakamiliza mechi ya mwisho Australia.
Matokeo ya kila mechi yalikuwa kama ifuatavyo.
Juni 13, 2014 : Uholanzi 5 vs Hispania 1
Magoli ya Uholanzi: Van persie dakika ya 44 na 72, Ruben dakiaka ya 53 na 80 na De vriji 64.
Ruben alimzalilisha Casillas, huku Van persie akipiga goli la kichwa cha kuelea.
Mechi ya pili Juni 18, 2014. Hispania 0 vs Chile 2
Magoli ya Chile: Vargas na Aranguiz.
Mechi ya tatu juni 23, 2014. Australia 0 vs Hispania 3.
Magoli ya Hispania. Villa, Tores na Mata.
Tusiogelee sana hiki kikosi cha Vicente del Bosque,
Tuchukulie umepewa nafasi ya kuchagua kikosi kibovu zaidi kati ya hivi viwili Ufaransa ya 2002 na Hispania ya 2014 kwa kupambanisha vikosi.
Unadhani kikosi kipi kitaubika na ushindi?
Na kati ya Barthez vs Casillas nani atakaa golini ukipewa nafasi ya kupanga vikosi kwa vikosi hivi viwili?
Watu wengi kipindi hiko walidhani hizo timu zingetetea ubingwa kulingana ukubwa wa majina wa wachezaji.
Lakini mwisho siku kilichotokea ni kinyume chake.
Ufaransa ya mwaka 2002 na Hispania ya mwaka 2014 zilishindwa kuvuka hatua za makundi.
Hata kabla ya kufikiria matokeo ya mechi walizocheza hebu kione hiki kikosi cha Ufaransa mwaka 2002.
Katika msimu wa mwaka 2001/2002 hawa wachezaji watatu wa Ufaransa waliongoza kwa ufungaji katika ligi za Ufaransa, Uingereza na Italia.
| Mchezaji | Klabu | idadi ya magoli | Ligi |
| Thiery Henri | Arsenal | 24 | Uingereza |
| Djibril Cissé | AJ Auxere | 22 | Ufaransa |
| David Trezeguet | Juventus | 24 | Italia |