Francesca Roja - Mmama aliyejulikana kama wakala wa shetani

Francesca Roja - Mmama aliyejulikana kama wakala wa shetani

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Tarehe 19 mwezi wa 6 mwaka 1982, katika makazi ya mwanamama ajulikanaye kama Francesca Roja katikamji mdogo wa Necochea, Argentina, kulitokea mauaji ya kutisha. Watoto wawili wa Rojas waliuawa kwa kuchomwa na kisu.

Yalikuwa ni mauaji ya kutisha sana. Rojas alidai kwamba, mwanaume mmoja aliyejulikana kama Velasquez ndiye anayemhisi kutekeleza mauaji hayo baada ya kuwa amemtishia maisha kwa kukataa kuwa na mahusiano naye. Aliendelea kudai ya kwamba wakati aliporudi nyumbani, alimuona Velesquez akitoka ndani ya nyumba yake na kukimbia.

Alipoingia ndani ya nyumba aliwakuta watoto wake ambaye wa kiume alikuwa na miaka sita na wa kike miaka minne, wakiwa wamechomwa visu na kupoteza maisha.

Bila kupoteza muda polisi walimkamata Velasquez. Lakini bwana huyu alikana kabisa kuwa yeye hakuhusika katika kutekeleza mauaji hayo. Polisi walimpa mateso sana ya kila namna ili akili uhusika wake. Lakini badi Velasquez aligoma kabisa kuhusika katika mauaji hayo.

Polisi walienda mbele zaidi kumweka katika chumba cha maiti alale na zile maiti za watoto usiku kucha labda atasema ukweli, lakini bado msimamo wake ulikuwa ule ule, hakuhusika na mauaji hayo. Polisi hawakuwa tayari kushindwa, waliendelea kutesa wka wiki nzima. Lakini jamaa aligoma kabisa kukili makosa.

Juan Vucetich, aliyekuwa kiongozi wa kitengo cha utambuzi wa wahalifu katika mkoa, alikuwa amevutiwa sana na habari za uwepo mbinu mpya ya kuwatambua watu kwa kutumia alama za vidole. Alimtuma kijana wake aende kuzungumza na mtaalam wa mbinu hiyo akaitaka kujua kama mbinu hiyo inaweza kusaidia katika kutambua mhusika.

Mtaalamu alifika na kuanza kuchunguza makazi ya Rojas, na alifanikiwa kukuta alama ya kidole gumba kwenye mlango wa chumba ikiwa na na chembe chembe za damu. Polisi walimwambia Rojas achukulie alama zake za vidole. Kupitia njia hii waligundua kuwa ile alama waliyokuta mlangoni inaendana na alama za kidole gumba cha Rojas. Kwa kutumia ushahidi huu Rojas alikuwa hana jinsi zaidi ya kusema ukweli.

Rojas, alikuwa akaua watoto wake ili apate nafasi ya kuolewa na mpenzi wake ambaye alikuwa amemwambia kuwa hakuwa akiwapenda watoto wake. Alimsingizia Velasquez akidhani kuwa polisi wasingetambua ukweli. Mwanamama huyo alichukiwa na kila mtu mpaka wengine kumpa jina la wakala wa shetani. Alihukumiwa kifungo cha maisha.

Hii ndiyo ilikuwa kesi ya kwanza ambapo matumizi ya alama za vidole yaliweza kutatua kesi. Forensic investigation kwa sasa imekua sana, DNA pia sasa wanaweza kudevelope profile kutoka kwenye mabaki madogo tu kuliko awali. Digital trail, sasa wanaweza kutumia simu yako kujua ulikuwa wapi, kujua mizunguko yako, wanaaweza utumia social media kujua ulichokuwa unafanya, Card za bank, wanaweza kujua kipi kiliendelea hasa kwa watu waliopotea.

Pia kumbe mapigo ya moyo yatofautina kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
 
Line ya mwisho inahusiana na hoja?
 
Line ya mwisho inahusiana na hoja?
Ni forensic investigation, ipo siku mapigo yako ya moyo yanaweza kutumika kukutambua pale ambapo watakosa finger pringt, au sura yako lakin kifaa kikanasa mapigo yako ya moyo. Maana kuna matukio mengi CCTV cameera ambazo uwa na quality mbovu zinanasa mharifu, lakini wanashindwa kumtambua sura
 
Licha ya teknolojia kukua bado inakua katika side mbili.

side ya mhalifu nao wamazidi kutumia teknolojia kubwa kukwepa mitego ya kukamatwa. N kinyume chake ni sahii
 
Back
Top Bottom