Francis Cheka aachiwa huru

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258

Bondia nyota zaidi nchini, Francis Cheka ameachiwa huru.
Cheka ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro. Lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo.

"Tayari ameachiwa, lakini tunashughulikia masuala kadhaa kumalizia ishu hiyo. Ila tayari yuko nje," alisema Kaike Siraju, promota wa ngumi za kulipwa aliyekuwa akipambana kuhakikisha Cheka anatoka.

Cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumtwanga na kumuumiza meneja wa baa yake mjini Morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara.

Chanzo: SalehJembe Blog

he! mbona haraka mno, hongera mahakama kwa kwenda fasta
 
Mahakama za nchi hii bwana..yaani rufaa imekuwa fast tracked?
 
Jela hata ufungwr siku moja ni adhabu tosha.

Taswira n hadhi yake imepigwa chini
 
Akaribie uraiani na ajaribu kuwa raia mwema, stress za maisha zisimfanye acommit crime!
 
Yule askari polisi aliyekula njama na hakimu wakampiga mvua sijui watakuwa wanajiskiaje. Anyway, kushinda kwa rufaa ni ishara kuwa adhabu haikuwa proportional na kosa. Wataalam wajifunze kutenda kazi kwa kutumia utaalam wao na sio mihemko au visasi.
 
Alifungwa kwa hujuma za kijinga .
 
Jera sitaki hata pasikia.
Ngoja niendele kuwa Law Abiding Citizen
 
cheka alihukumiwa bila kusikilizwa. Rufaa imetenda haki.
 
Yule askari polisi aliyekula njama na hakimu wakampiga mvua sijui watakuwa wanajiskiaje. Anyway, kushinda kwa rufaa ni ishara kuwa adhabu haikuwa proportional na kosa. Wataalam wajifunze kutenda kazi kwa kutumia utaalam wao na sio mihemko au visasi.

Ndio maana kuna rufaa ili kurekebisha makosa. Hata ukitoa rushwa jamaa anakuridhisha, halafu anajua aliyeumia akienda kwenye rufaa anashinda. Lakini imemtoka mikononi mwake aliyehukumu na kuchukua kitu kidogo.
 
Mkuu rufaa sawa ni haki ya kila mtu, lakini kwani kuna haja ya kuboronga kwasababu tu kuna chance ya rufaa?
 
Kimsingi amesamehewa tuu mlalamikaji ameridhika asamehewe kwa hiyo njia pekee ilikuwa ni kupitia njia ya rufaa.
 
mimi nipata kueleweshwa
kumbe ukifungwa bado unao uwezo wa kukata rufaa??
na je, ukiwa ndani nani hasa atakua anakisaidia kukata??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…