Anaandika Mwanasheria Garatwa Francis
Awali ya yote nitumie nafasi hii kumpongeza mtaalam wa Idara ya IT - Makao Makuu ya CHADEMA Taifa, kijana mwenzetu Remigius Selestine kwa ujasiri wake wa kuamua kuueleza umma kupitia maandiko yake yanayobebwa na kichwa habari; MAPIGO 10 LISSU VS MBOWE.
Hakika, ni wataalam wachache sana wenye uthubutu wa kiwango hiki alichokionyesha huyu mpambanaji Remigius Selestine. Wengi huishia kuwa wanafiki kwa sababu ni wafuasi wa watu badala ya taasisi na badala yake chama kinapoumizwa wanabakia kuwa watazamaji tu pasi na kuonyesha umma usiojua lipi la kufanya na mwisho wa siku taasisi inakufa ndio wanaamza kusema sisi tulijua hayo yatatokea.
Natambua Remigius anayo MAPIGO 10 mfululizo na kati ya hayo MAPIGO 10 aliyonayo, tayari Remigius ameshatoa MAPIGO (3) MATATU ambayo yanaendelea kuupa umma mwanga wa wapi tulipotoka kama Chama, ni wapi tulipo sasa na ni wapi tunakopaswa kuelekea. Hongera sana mpambanaji Remigius 👏
1. HOJA YA YERICKO KWAMBA, LISSU HAGOMBEI KWA UAMUZI WAKE
Uamuzi wa Tundu Lissu vyovyote ambavyo ungepaswa kuwa; ieleweke wazi kwamba, kama akina Yericko (team mbowe) wamegundua kwamba; Lissu ANAGOMBEA kwa uamuzi wa watu na sio uamuzi wake, wanapaswa pia kuelewa kwamba, watu wamelazimika kumuomba Lissu ili wamtume akasimame kwa niaba yao kama Mwenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa kwa sababu wamempima na kuamini pasi na shaka kwamba, yeye ni mtu sahihi kwa sasa ukimlinganisha na huyu Freeman Mbowe wa sasa.
Sio kosa, sio dhambi wala sio haramu watu wakiamua kumuomba mtu ama kumshawishi kushika nafasi fulani ya kiuongozi ndani ya taasisi. Hata mimi Garatwa nimewahi kuombwa na watu wa nyumbani kwetu nigombee Udiwani kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili hali kipindi hicho nilikuwa Mwenyekiti wa Kijiji na nikashinda nikawa Diwani wao mpaka Mwendazake alipofanya yale yake
Kitendo cha watu kumuomba Lissu abadili nafasi yake ya mwanzo na agombee Uenyekiti wa Chama ngazi ya Taifa ni ISHARA tosha kwamba, Lissu anaaminika kwa sasa mbele ya wanachama na wapenda mabadiliko wote waliopo ndani na hata nje ya nchi hii. Mfano mzuri katika hili ni uungwaji mkono anaoupata Lissu kutoka kwa watanzania wenzetu wa Diaspora.
Hata Mbowe mara zote amekuwa akisema kwamba, nimegombea kwa sababu ameshinikizwa na watu pasipo uamuzi wake yeye mwenyewe.
2. HOJA YA YERICKO KWAMBA, DIASPORA NDIO WANAOANDAA VIKAO VYA LISSU
Hoja sio vikao.vya Lissu vinaandaliwa na nani Brother Yericko. Hoja ilishageuka sasa inahojiwa kwamba, ni kwa nini wale Diaspora waliokuwa wanamuamini Mbowe; hivi sasa hawataki tena hata kumsikia na hata wao wanamtaka Lissu awe Mwenyekiti wa Chama ngazi ya Taifa?
Yaani Diaspora waliokuwa wanatembelewa na Mbowe ikiwemo kule London nchini Uingereza, leo hii hawataki kabisa kusikia habari za mtu anayeitwa Mbowe aendelee kuiongoza CHADEMA kwa miaka mingine mitano na wanamuunga mkono Lissu na hata timu Mbowe akiwemo Yericko wamejua hilo kwamba, Diaspora wanashiriki kufanikisha hata vikao vya Lissu.
Automatically, kwa wanaotazama mbali na pale walipokanyaga, haya ni malalamiko ya kuzidiwa mbinu za vita mapema na hatua hii ya Diaspora kumkataa Mbowe hadharani na kumuunga mkono Lissu inaonyesha wazi ni kiwango gani imewachanganya team Mbowe na hata Mbowe mwenyewe na ndio maana unaweza kuona watu aina ya Yericko ambao ni wanazi wa kufa na kuzikana na Mbowe wanavyolalamika hadharani.
Sisi tunaamini Diaspora ni Watanzania wenzetu ambao ni wapenda mabadiliko tena wanaojitolea sana hata kifedha kusaidia shughuli za ujenzi wa Chama na hata zile shughuli za kiutendaji ndani ya Chama. Utofauti wetu na wao ni kwamba, sisi tunaishi ndani ya nchi; ila wao wanaishi nje ya nchi..
Hivyo basi, wenzetu wa Diaspora wanastahili kuheshimiwa na kupewa thamani yenye viwango sawa na wengine katika kushiriki kwenye shughuli za ujenzi wa demokrasia kwenye nchi yao; lakini pia mawazo na mitazamo yao kuelekea nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa iheshimiwe kama ilivyokuwa huko nyuma wakati wanamuunga mkono Mbowe; na watu walioko nyuma ya Mbowe wasipotoshe umma kwa kutaka kuwatfsiri vibaya watanzania wenzetu wa Diaspora kisa tu kwamba; hivi sasa wao hawana imani tena na Mbowe kuendelea kukiongoza tena chama.
Mbona walipokuwa wanamuunga mkono Mbowe na kutuma mpaka michango ya fomu yake enzi hizo zote hawa akina Yericko Nyerere hawakuona kama ni wabaya. Ubaya wa wenzetu wa Diaspora ni upi? Kwa ni timu Mbowe muwaone Diaspora kama ni haramu ama maadui kisa wameamua Chama kibadilishe mfumo wa uongozi kwa kuachana na Mbowe apumzike na Lissu ashike nafasi?
Ukweli ambao hausemwi hadharani ni kwamba; Lissu anaungwa mkono kila mahali kwa sasa iwe ndani ya nchi na hata nje ya nchi kupitia watanzania wenzetu wa Diaspora wanaoishi mataifa mbalimbali duniani kote.
Hata kule kwetu Mkoani Mara; sisi Wakurya hatuna mawaaa. Kwetu nyeupe ni nyeupe na kama nyeusi huwezi kutuambia tuseme ni njano. Ukitaka iwe hivyo unavyotaka; ujue patachimbika na lazima tutoane meno bila ganzi.
Ieleweke wazi na kwa kila mmoja kwamba; tuko nyuma ya Tundu Lissu. Akishindwa tutashindwa wote na Lissu akishinda tutashinda wote
3. LISSU AMEBADILI NAFASI ANAYOGOMBEA KWA SHINIKIZO/USHAWISHI
Huyu mtaalam wa Mizimu ya Mababu wa Mbutu Yericko Nyerere, anasema Lissu ameamua kubadili nafasi yake aliyotaka kugombea mwanzo kwa sababu za shinikizo. Sitaki kuwa msemaji wa Lissu; lakini kwa sababu yeye mwenyewe alizungumza hadharani, naweza kupata kibali chake cha moja kwa moja kusema kwa niaba yake.
Kama hoja ni Lissu kupewa ushawishi ama shinikizo; mbona hata huyo Mbowe mara zote amekuwa anasema nilikuwa sitaki kugombea ila nimeombwa na watu na nimejikuta naletewa fomu nyumbani. Sasa kama Mbowe enzi hizo alikuwa anajikuta amepelekewa fomu nyumbani 😄 kuna tatizo gani kama Lissu na yeye akishinikizwa ama akashawishiwa na watu ili agombee. Ama kama vipi; awamu hii na Lissu achukuliwe fomu ya kugombea kama tulivyokuwa tunafanya kwa Mbowe; kwani shida iko wapi kama sisi ndio tunaotaka awe Mwenyekiti?
Kwani huyo Mbowe kama isingekuwa watu kumshinikiza na kumshawishi; angekuwa Mwenyekiti mpaka sasa. Achilia mbali huko nyuma, mbona sasa hata wewe Yericko Nyerere unasema utamwambia agombee na unasema hadharani kwamba wewe ndiye utalipia fomu yake. Huko sio kushawishi ama hilo sio shinikizo?
Kunya anye kuku ila bata akinya ameharisha, hiyo ni sahihi? Hii hapana. Zama zilishabadilika sana. Hata Lissu ana watu; tena hivi sasa Lissu ana watu wengi sana kwa maana ya wajumbe halali wanaopiga kura kumzidi Mbowe. Hivyo basi, hata Lissu anayo haki ya watu kumuomba agombee Uenyekiti wa Chama; Lissu anayo haki ya kushawishiwa na watu na vile vile Lissu anayo haki ya kupata shinikizo la watu ambao wanaamini yeye ni the best candidate kuliko Mbowe kwa sasa kuelekea mtanange huu wa nani anatufaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Kwa mazingira ya siasa za sasa, hakuna namna tena. Tunamhitaji mtu mwenye karba na stamina ya kisiasa kama Tundu Lissu na ndio maana timu Mbowe wanashtuka kuona Lissu anavyopata ushawishi kutoka kwa watu wengi wakiwemo watu wa maana sana kwenye mageuzi ya nchi hii; namaanisha watanzania wenzetu wa Diaspora.
Zama za busara na hekima za Mwenyekiti zimepitwa na wakati sasa. Tazameni Chama kinavyokwenda goi goi hivi sasa. Utadhani ni kikundi fulani hivi cha wahuni. Kibaya zaidi, wanufaika ni wale wale wanaomkumbatia mfalme juha.
Lakini pia, Lissu alijieleza vizuri sana mbele yetu sisi wanachama kuhusu sababu zake za kwa nini ameamua kubadili nafasi yake ya mwanzo ya Makamu Mwenyekiti na akaamua kuandika barua ya kugombea Uenyekiti wa Chama na hakuna mahali popote pale ambapo Lissu alisema ameshinikizwa kuhama nafasi yake ya mwanzo.
Kupitia maelezo yake, sisi wanachama nikiwemo mimi Garatwa tulimuelewa vizuri sana na ni kwa bahati nzuri kwamba, Lissu ndiye aliyekuwa hitaji letu tulio wengi kwenye hiyo nafasi maana tulishaona miyeyusho mingi sana kwa huyo Mwamba wenu. Yaani kitendo tu cha Lissu kutangaza kuhamia kwenye Uenyekiti wa CHADEMA Taifa, kuna watu mamillioni kwa mamillioni walipata tumaini jipya la kesho yao maana hali ilishakuwa sio hali ndani ya hiki chama asikwambie mtu.
Anayebisha katika hili anyooshe mkono wake juu tumuone. Ukweli mchungu usiopendwa ni kwamba, kuna watu maelfu kwa malaki walishakata tamaa na kurudi nyuma kwa sababu ya mwenendo wa chama chini ya Mbowe na ndio maana hata yale maandamano ya Magomeni yalipoitishwa, Mbowe alikuwa peke yake na kama mliona vizuri wakati anakamatwa, alikamatwa kama kuku tena na askari mmoja tu; huku akivutwa kama mhuni tu wa mtaani.
Hawa watu sio wajinga, wanaweza wasiweze kusema kwa njia ya maandiko kama akina Yericko, Garatwa, Malisa na wengine wengi tunaosema kupitia maandiko yetu, lakini kwenye vitendo ikifika siku husika watasema kwa TIKI ZAO ZA NDIO KWA TUNDU LISSU na mkakati wa kuinusuru CHADEMA kutoka kwenye makucha ya wapiga dili utakuwa umekamilika.
Mbowe amepoteza ushawishi kwa sababu ya mienendo yake yenye mashaka dhidi ya vikao vyake vya siri na Mama yenu. Lissu amekuwa imara sana wakati wote pamoja na hali zake za kiuchumi anazosema Yericko kwamba anategemea wafadhiri, lakini bado hajawahi kuwa vuguvugu ama mtelezo kama mlenda.
Lissu ndiye suluhisho kwa sasa. Tunafahamu ni jinsi gani wale Covid 19 wanavyopambana hata kwenye chaguzi za Kanda ili watu waliopo kwenye channel ya Mbowe washinde ili wapate ahuenu ya kurudi kwenye chama maana hata watu walioko nyuma ya Mbowe pale Makao Makuu ya Chama, sehemu kubwa ya wenye maguvu ni waume na wapenzi wa wale Covid 19.
4. LISSU HAJAWAHI KUITUMIKIA NAFASI YOYOTE ILE YA KIKATIBA
Katika muendelezo wangu wa kumsoma Yericko Nyerere kupitia andiko lake, nimeona anasema; Lissu hajawahi kuitumikia nafasi yoyote ile ya Kikatiba na kwa mujibu wa maelezo yake, ametaja nafasi ya Mkurugenzi wa Sheria CHADEMA Taifa na amesema kwamba, Lissu hajawahi kuitisha vikao vya Kamati yake ya Maadili kama Makamu Mwenyekiti wa Chama.
Kwanza, tukubaliane kwamba, katika hili; Yericko amezungumza mambo ya kusikia na kuambiwa na watu kwa sababu yeye sio sehemu ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama na hajawahi kuwa sehemu ya vikao hivyo maisha yake yote.
Ukimuuliza ulijuaje hizo habari za vikao vya Kamati Kuu unazozieleza hapa ili hali wewe sio mjumbe wa vikao hivyo vya Kamati Kuu, ataishia kukwambia; tunasikia watu wanasema ama utashangaa anakuuliza kwamba; kwani wewe hujui? Kifupi Yericko anatumia hearsay (maneno ya kuambiwa) ama rumors (uzushi) kutaka kupotosha watu ili wamuamini Mbowe maana amesema yeye anataka akailipie fomu yake na amwambie agombee.
Kama Lissu hajawahi kuitisha vikao vya Kamati yake kama Makamu Mwenyekiti, mimi binafsi Garatwa ninavyomjua Lissu alivyo very smart kwenye masuala ya kiutendaji, lazima zipo sababu zenye mashiko sana katika hili na ninaamini ipo siku moja Lissu atasema mengi yaliyomo kifuani mwake.
Aidha, nimeona Yericko anasema kuhusu masuala ya Lissu kwamba aliwahi kuwa Kiongozi wa Kanda hakufanya vikao. Katika hili kidogo nimepata mashaka na mtaalam wangu wa maandishi na fasihi; Yericko ambaye nasoma sana vitabu vyake. Nimejiuliza kwamba, ina maana Yericko hajui protocol za uitishaji wa vikao ndani ya Chama chetu zilivyo? Ina maana hata vikao vya Kamati Kuu vinaitushwa na Mbowe? Please Brother, hebu jaribu kuwaambia watu vitu vyenye hoja za maana na sio hivi vitu vya ajabu hasa kwenye nafasi kama hii ya Uenyekiti wa Chama ngazi ya Taifa.
Yericko, ni kweli unaamini kwamba, Lissu hawezi kuwa na maelezo yenye ukweli usio na chembe za shaka kuhusu hizi hoja zako Brother. Ukitaka unishukuru na kunielewa nasema nini, hebu jaribu kumuuliza Lissu ilikuwaje halafu umsikilize. Naamini anaweza kukupa kabisa hata na uthibitisho wa atakachokueleza.
Personally! I believe that; Lissu is a professional who is very smart enough Brother Yericko.
Sisi tujikite kumpigia kura ashinde hii nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa; halafu mengine mengi tutayaona akiyasahihisha kwa vitendo na tutambue kwamba, ili AGANO hili lipate kutumia, ni lazima Lissu asemwe kwa kila jambo; na lengo kuu ni ili hilo genge la watu kadhaa tunaowakataa kwa sababu za madudu yao lipate nafuu ya kuendeleza upigaji kwenye hii taasisi. Tuukatae uhuni huu kwa kuomba kura za Lissu kwa wajumbe wengi zaidi.
5. LISSU NI MUONGO NA SIO MKWELI KWA WANACHAMA
Kama ni kuna uwezekano wa kuongeza ajabu la (8) nane kwenye ile orodha ya maajabu (7) saba ya dunia; basi sisi Tanzania tuombe dunia iongeze hii kauli ya Yericko Nyerere kwamba, Lissu ni muongo kwa wanachama. Uongo wa Lissu ni upi ambayo wengine hatujawahi kuusikia isipokuwa Yericko peke yake? Au ni kwa sababu Yericko anaamini katika mizimu na wengine tunaamini katika uwepo wa Kristo na Mtume Mohammad? Naomba Yericko asaidie maana binafsi naona kabisa hii mizimu ya ukoo wao huko Mbutu Kigamboni haitamuacha salama awamu hii.
Yericko anasema Lissu aliwadanganya wanachama kwamba, CHADEMA hatukupata chochote kwenye maridhiano ili hali tulipata Mikutano, Wafungwa wa kisiasa waliachiwa, Wafanyabiashara walipewa pesa zao walizoporwa; lakini hapo hapo anakubali hadharani kwamba, kupitia hayo maridhiano CHADEMA ilipoteza mambo muhimu ambayo ndio yaliyobeba vipaumbele vikuu vya Chama ambayo ni Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, Mabadiliko ya Sheria mbalimbali na Tume ya Uchunguzi wa Mauaji.
Sasa mimi najiuliza, huo uongo wa Lissu anaousema Yericko uko wapi. Kama Lissu anasema tumepoteza vyote kosa liko wapi ili hali vipaumbele vya Chama vyote hakuna hata kimoja ambacho kimefanikiwa?
Kwani malengo ya kupata Katiba yalikuwa ni yapi? Ama Yericko yeye hajawahi kuujua umuhimu wa Katiba Mpya kwamba, Katiba Mpya ndio ingesidia kuondoa hizi hisani za mambo ya msingi ambayo yapo Kikatiba. Ina maana Yericko yeye hajui kama Katiba Mpya ingepatikana tungepata mifumo imara isiyo ya kupiga magoti kama anavyoona kwamba magoti tunayopiga na kunyenyekea kwa Mbowe mbele ya hii CCM na dola yake kunapaswa kuendelezwa tena na Mbowe kwa miaka mingine (5) mitano mbele. What a shame Brother Yericko?
Kitendo cha kukosa Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na Mabadiliko ya Sheria mbalimbali zikiwemo za Uchaguzi na ile ya Vyama vya siasa, kimekuwa chanzo cha watu wengi akiwemo Yericko kuendelea kuamini kwamba; busara za Mbowe na upole wake wa kunyenyekea mbele ya Mwenyekiti wa CCM unaweza kuifanya hii CHADEMA ya sasa iliyolala chini dhoofu ili hali iweze kuinuka tena.
Tazameni tunavyofanywa kwenye chaguzi za Kiserikali kwa misimu miwili mfululizo ya uchaguzi chini ya uongozi wa huyu huyu Mbowe mwenye busara.
Mapambano ya kisiasa kwenye nchi yalipofikia hivi sasa, yanamhitaji mtu mwenye msimamo wa maana sana kama Lissu; Busara za Mbowe na Upole wake vimetuponza na ukitazama vizuri na kwa umakini, utagundua kabisa kwamba, CHADEMA inazidi kupoteza uungwaji mkono na hata watu wa ndani kwa sababu ya uongozi kuwa na kimazoea na kishikaji sana.
Lissu ni dawa na suluhisho la kudumu kwenye matatizo haya. Lissu anaamini zaidi katika mifumo imara ya kitaasisi inayofuata na kuzingatia utawala wa Sheria na ndio maana CCM hawataki kusikia Lissu anakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na wanamtaka Mbowe ili waendelee kunufaika na hizo hekima za mfalme juha.
6. SUALA LA PESA ZA ABDUL WA MAMA YENU.
Nimeona Yericko amelizungumzia kiwepesi sana suala hili ambalo ni hatarishi sana kwa ustawi wa chama kwa ujumla. Hata bila aibu, Yericko anajaribu kuuhadaa umma kwa kutaka kuupindisha ukweli wa wazi kabisa ambao Lissu mwenyewe alishaueleza wazi. Yericko anajaribu kutumia hoja ya email za kutuma nyaraka kama kigezo cha kukwepa ukweli kwamba, kuna ushenzi mwingi sana wa kupiga pesa za dola kwa mgongo wa Chama.
Labda nimuulize Yericko mambo kadhaa hapa; kwani wakati Lissu anaeleza kuhusiana na mkasa mzima wa haya mambo mgao wa Abdul, hakusema suala la nyaraka kwamba yeye ndiye aliyewagomea ombi lao la kutaka achukue mgao wake na badala yake akawaambia kama mnataka kunisaidia pesa ya kununua gari la kutembelea kama mnavyosema;
Nipeni zile za halali nilizotibiwa baada ya kuumizwa na akatoa nyaraka akampa Abdul. Ushahidi wa haya ninayoyasema huu hapa kwenye hii Link Leo mchana nimeona clip ya video ya Mama mmoja hivi wa BAWACHA online akielezea mazingira ya kutekwa kwake. Kwa sababu ni ule ule muendelezo wa siasa za... | By Garatwa | Facebook unaweza kubonyeza usikikize mwenyewe halafu uchanganye na hizo za kuambiwa na Yericko Nyerere.
Kifupi ni kwamba, kitendo tu cha huyo anayeitwa na Yericko kwa jina la Kiongozi wa CHADEMA na Mfanyabiashara mkubwa wa ndani na nje kuingia mseto na mtoto wa Mama yenu kuhusu mambo yenye sura ya kisiasa; ni hatari kubwa sana japo Yericko kwa kuwa anazungumza kwa mahaba ya kumchukulia Mbowe fomu ya kugombea yena Uenyekiti baada ya miaka 20, hawezi kuona hilo kama ni chochote.
CCM hawataki kusikia Lissu anakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na wanamtaka Mbowe ili waendelee kunufaika na hizo hekima za mfalme juha.
7. KWAMBA, LISSU HAWEZI KUPATA MISAADA YA UENDESHAJI WA CHAMA.
Kwani Mbowe anapewa hiyo misaada na nani huyo ambaye hawezi kutoa kisa Lissu anaiongoza CHADEMA na sio Mbowe? Kwani hiyo misaada ni misaada kwa ajili ya taasisi yaani CHADEMA ama ni misaada binafsi kwa ajili ya Mbowe na familia yake kule Machame mpaka Lissu asipewe kisa Mbowe sio Mwenyekiti?
Kwani hivi sasa kati ya Lissu na Mbowe ni yupi ana ushawishi mkubwa hapa ndani na hata nje ya nchi especially mbele ya Wafadhiri na hata mbele ya watu wa Diaspora kuliko mwingine kama tukiamua kuusema ukweli?
Yericko mwenyewe kupitia hilo andiko lake, amekiri wazi kwamba, watu wa Diaspora kwa sasa ndio wanaomtaka Lissu agombee Uenyekiti wa Chama. Sasa kama Diaspora wanamuunga Lissu mkono na sio Mbowe hatuoni kama Lissu anakwenda kuleta manufaa makubwa kwenye chama kuliko Mbowe ambaye kwa sasa amepoteza ushawishi na kiwango cha kukubalika kwake kinazidi kushuka kwa kasi ya ajabu hususani jinsi watu wanavyoendelea kuupima mwenendo wake sasa na ule wa miaka iliyopita.
Huyu Mbowe wa sasa wakikutana na yule Mbowe wa miaka iliyopita, watagombana na kulaumiana sana maana Mbowe wa zamani atashangaa kuona chama kinavyoongozwa kihuni hivi sasa.
Sura ya (8) nane ya Katiba yetu ya Chama ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2016 imeeleza wazi njia rasmi za Chama kupata fedha za kujiendesha, nanukuu kwenye Katiba ya Chama kama ifuatavyo;
Ibara ya 8.0 inaelezea kuhusu MAPATO, MALI NA WADHAMINI WA CHAMA:
(a) Ada na viingilio vya wanachama.
(b) Michango ya hiari ya wanachama na wafuasi
wa Chama.
(c) Michango ya hiari ya watu wa ndani na nje wanaounga mkono Chama ndani na nje ya
nchi.
(d) Misaada na Ruzuku toka ndani na nje ya nchi.
(e) Mapato yanayotokana na hisa na miradi
halali ya Chama.
Hivi ndivyo vyanzo ambazo Lissu na timu yake mpya watakwenda kuvisimamia na kuviboresha zaidi ili kupata fedha za kuendesha chama. Yericko anajaribu kuhadaa watu kwa uongo wa wazi kwamba, Mbowe ndiye ana misuli ya kifedha ya kuweza kukiendesha chama ili hali wote tunajua Mbowe na waliomzuguka wamekikamua na wanaendelea kukikamua chama mpaka chuchu zake zinauma sana hivi sasa.
Yericko anapotosha umma kwamba, anauwezo kugharamia mikutano na vikao lakini sio Lissu. Uongo uliokubuhu huu, nani asiyejua michezo wanayoifanya akina Mbowe na waliomzuguka. Pesa inakopwa kwa jina la Mbowe, Chama kinatumia kama deni, halafu Mbowe anatukuzwa amesaidia yeye. Acheni kuendelea kutuona mazwazwa wa kiwango hicho.
Awamu hii tumesema, hata Lissu na yeye anaweza kukopa kwa jina lake kama Mwenyekiti wa Chama halafu Chama kikalipa hilo deni; na akabeba sifa kama Mbowe anavyotukuzwa kwamba yeye ndiye anayetoa pesa kumbe chama kinakopeshwa na baadae kinalipa madeni.
Garatwa Francis,
Dar es Salaam, Tanzania.
16 Disemba, 2024.