Aligombea nafasi za kisiasa kupitia chama kongwe cha CCM, hiyo imeleta mtafaruku ktk jukwaa hili la wafanyabishara Tanzania
9 Jul 2020 — Chanzo chetu kinabainisha kuwa aliyekuwa kiongozi wake mkuu, Francis Nanai alikuwa akilazimisha habari za kuibeba serikali, na CCM .....
Nanai alitangaza kujiuzulu Juni 30, 2020.....
alikuwa akitajwa kulazimisha aina ya story za kwenda, nyingi zikiwa zimechujwa kwa kiwango kikubwa.
Je, Mainstream Media yetu iko salama?
===
Kampuni ya Mwananchi kukwama zaidi. Nanai ang’atuka
Kushuka kwa mapato ya mauzo ya gazeti la Mwananchi na kuzuiwa kwa matangazo mengi toka taasisi na mashirika ya umma na serikali kunaongeza uchungu katika mlolongo wa changamoto za ustawi wa gazeti hilo kwa sasa.
Kwa muda mrefu sasa, gazeti hilo limekuwa likichechemea kiuchumi huku taarifa za ndani zikionyesha kuwa limeanza kuelemewa na madeni yanayotokana na gharama za uendeshaji, hasa uchapaji. Gharama kubwa katika uchapaji zinahusisha ununuzi wa karatasi, wino, umeme na usafirishaji. Pia zipo gharama za uendeshaji....