FRED katikati ya Ushujaa na Kiza cha Kesho

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Ukiitaja Manchester United kwa Kipindi cha msimu huu na wachezaji wake waliocheza kwa kiwango cha juu hutasita kulitaja jina la mbrazili Frederico Rodrigues maarufu kama Fred akivalia jezi nambari 17 mgongoni.

Yupo na alikua kwenye kiwango bora sana tofauti na ilivyoonekana mwanzo kwamba ni hasara ya makusudi kwa klabu ya United na hata mkufunzi Jose Mourinho aliyekua akiinoa Manchester United kwa wakati huo akadiriki kusema kiungo huyo alishapoteza ubora wake.

Akiwa na asilimia 54 za kucheza mipira ya kulala yombo (tackling) anakua mmoja kati ya viungo wenye wastani mzuri kati ya viungo wanaocheza kwa eneo lake ingawa bado hana wastani mzuri mbele ya msitari wa kati kati ya uwanja kwenda mbele kwani kasaidia upatikanaji wa mabao manne tu kwa mlengo wa moja kwa moja kwenye ligi kuu nchini Uingereza ila amejidhihirishia ushujaa mkubwa kwenye akili za mashabiki wa United na kuwasahaulisha hasira zao dhidi ya Paul Pogba ambaye hatma yake haifahamiki ndani ya timu.

Ameibuka kuwa bora ilhali miezi 10 iliyopita aliishi kama mtoto wa kambo ndani ya Manchester United, Fred atakimbia kulia ataenda kushoto ataenda nyuma Kisha atasogea kati kati kwenda mbele kusaidia mashambulizi kwa wakati. Amechagua maisha hayo na hukosei sana kusema "jiwe walilokataa waashi limekua jiwe kuu la pembeni".

Anavutia kumtazama namna anavyokimbia huku na kule akiwania mpira na kuwasogezea wenzie kwenye nafasi huku akiwa kwenye kiwango bora kadri michezo ilivyokuwa inasonga mbele.

Upigaji wake mashuti sahihi kwa asilimia 19 unamfanya kuwa miongoni mwa viungo wasio na shabaha sana ingawaje kadri siku ziendavyo anaonekana kuimarika katika eneo hilo na huenda atafanya makubwa zaidi.

Mwezi Januari klabu yake ilimuongeza Bruno Fernandez kikosini, huyu ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana pale Uingereza kwa sasa ingawaje bado ni mapema na alivyofika tu akacheza na Fred, Scott ama Juan Mata kwenye eneo la kiungo na waliifanya United kuwa tishio kwa muda mfupi huku Fred akiendelea kudhihirisha ubora wake.

Kwa sasa Paul Pogba amerejea kikosini. Pogba mara zote ni mchezaji wa kikosi cha kwanza na lazima atacheza na Bruno kazi inabaki kwa Fred na Scott kuchuana nani atacheza na hawa wawili labda kama Solskjaer meneja wa United atumie mfumo wa 4-1-3-2 ili Fred, Pogba na Bruno wacheze juu ya Scott au Nemanja Matic ambao bila shaka wana uhakika na eneo lao. Hapo ndio naona kiza kwa Fred na nafasi yake.

Huenda akarudi kukaa benchi tena ama akacheza tena kiungo cha chini jambo ambalo linaweza kuifanya United ifanye makosa mengi kwenye eneo lao na kujikuta ikiadhibiwa, Mzigo utamwangukia Fred.

Ni ngumu kubashiri ila naona kama ni wakati wa Olle, Michael Carick na Mike Phelan kupagawa zaidi hasa kwenye eneo la kiungo. Asuke ama anyoe sasa ni jukumu lake Olle.
Wasalaam
 
Inabidi waanze FRED, POGBA, BRUNO na MATIC.

Huko mbele RASHFORD na MARTIAL
 
Fred inatakiwa awe mtu wa kwanza kutajwa when CDM is concerned
 
Ame'improve' sana kwakweli. Ilikuwa ukimuona kikosini tu unalaumu lakini kwasasa asipokuwepo unalaani. Kikubwa tunachoombea ni 'consistency'.

Ggmu
 
Ame'improve' sana kwakweli. Ilikuwa ukimuona kikosini tu unalaumu lakini kwasasa asipokuwepo unalaani. Kikubwa tunachoombea ni 'consistency'.

Ggmu
[emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…