Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mfanyabiashara maarufu, Fred Vunjabei amemtolea uvivu Mwijaku na kumtaka aache kumhusisha na ishu za utajiri, baada ya Mwijaku kudai kuwa Fred ana utajiri mkubwa kuliko Diamond Platnumz, wakati akipinga ndoto ya Diamond ya kuwa tajiri namba moja duniani.
Fred, mmiliki wa kampuni maarufu ya mavazi ya Vunjabei, ameonya kuhusu matumizi ya jina la kampuni yake mitandaoni, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu biashara na mahusiano.
Pia katika andiko lake amefichua kuwa amewahi kumfungulia Mwijaku mashtaka, ingawa suala hilo liliisha kwa makubaliano, lakini sasa ameomba Mwijaku akome mara moja kumtaja au kampuni yake, "vunjabei", kwenye mijadala yake ya mitandaoni.
Baba Levo, mmoja wa watu wa karibu wa Diamond, naye pia alijitokeza kumpinga vikali Mwijaku, akionyesha msimamo wake kuwa Fred na Diamond wanastahili heshima.
Soma Pia: Mwijaku kayatimba, Diamond Platnumz amjibu ataka mdahalo kuonesha utajiri iwe funzo