Rich Pol
JF-Expert Member
- Oct 11, 2013
- 7,874
- 5,685
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela mwishoni mwa wiki iliyopita alichukua fomu ya kuwania ridhaa ya ubunge wa Jimbo la Iringa mjini na kuwatahadharisha wenzake kuacha siasa za majitaka zinazofanywa na baadhi ya watangaza nia.
Mwakalebela ambaye mwaka 2010 alijitosa kuwania ubunge katika jimbo hilo ambapo alikusanya idadi kubwa ya waliomshabikia na kumhitaji lakini kutokana na baadhi ya changamoto zilizojitokeza alishindwa kuwatumikia alisema bado ana dhamira ya kuwatumikia Iringa mjini kwa sababu bado ana dhamira ya kweli kuwaletea maendeleo wakazi wa jimbo hilo.
Alisema siasa za majitaka zitasababisha kuligawa jimbo hilo kwa Wapinzani ambao macho na masikio yao wameyatega katika chama hicho kinachoshikilia dola.
Mwakalebela alisema Iringa mjini kuna changamoto nyingi ambazo zinatakiwa kutekelezwa kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hivyo wao kama wagombea wazingatie ilani hiyo ili kutolipoteza kwa mara nyingine jimbo hilo.
Aidha Mwakalebela alisema iwapo atashindwa kupata ridhaa ya wakazi wa Iringa Mjini yuko tayari kutoa ushirikiano kwa atakayefanikiwa kupata ridhaa kwa sababu wana CCM wanatakiwa kuwa na nguvu moja ambayo inatakiwa kupata ushirikiano.
Nachukizwa na siasa za majitaka kwa sababu hazitusaidii hasa kwa changamoto tulizonazo ambazo zinatakiwa kutatuliwa na watia nia kama Mwakalebela na wengine ambao wana dhamira ya kufikia ujumbe wa jamii bungeni, alisema Mwakalebela.
Mwakalebela mwenye marafiki Uswisi, Australia, America, Denmark, Qatar, Hispania na Scandinavia anajitakasa kupitia mafanikio aliyoyatekeleza alipokuwa TFF ametoa wito kwa wakazi wa Iringa kutofanya makosa kama yaliyotokea mwaka 2010.
Mwakalebela aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuwania ridhaa hiyo aliyoichukua CCM Mkoani Iringa ambako alilakiwa na mashabiki lukuki waliojitokeza kumsindikiza.