Fredrik werrema akiri prof shivji, dr benson bana ni makini kuliko baadhi ya wabunge,

Fredrik werrema akiri prof shivji, dr benson bana ni makini kuliko baadhi ya wabunge,

Future president

Senior Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
144
Reaction score
39
Mwanasheria mkuu fredrik werrema akiwa anahojiwa na star tv tarehe 09/02/14 amekiri prof shivji,dr benson bana ni watu makini kuliko baadhi ya wabunge,sasa nashangaa kwanini hawakuwachagua katika bunge la katiba,hawa jamaa mbona ni wanafki sana,wanania gani na taifa hili,mnatutaka nini watanzania,mnajisahau na kuanza kuropoka vitu ambavyo mliviacha katika zoezi kama hili la katiba,eti anasema hana chama kweli kweli werrema huna chama aaaah!!!? Hutaki wana cccm wasitaje mawaziri mizigo,kweli huna chama mbona unakisemea chama!?
 
Ngoja niendelee kuichambua habari ya Dail Maily tu maana huyu mwanasheria nae ndo wale wale tu hivi nae ni kati ya wale wanaojiita Wasomi?
 
Kosa lilianza pale kwenye Tume ya jaji Warioba sielewi mtu mwenye mchango mkubwa kama Profesa Shivji aliachwa kuna hofu gani kwa profesa huyu mwanazuoni makini?
 
werema amekili kuwa yeye wakati anasoma alikuwa mwenyekiti wa TANU jumuiya ya vijana na kweli ingawa ni mwanasheria mkuu wa serikali ana mapenzi makubwa kwa CCM
 
Bunge lenyewe limejaa watu wengi wa kada yake hapakuwa na sababu ya kuteua wote, kuna kosa bwana mkubwa alilolifanya kwa kuteua wanazuoni wawakilishi wa elimu ya juu na kusahau wanazuoni wa kada ya uanafunzi!

Kuna wakati nilikuwa natafakari nikafikiri pia asilimia kubwa ya watu walioteuliwa kwenye hili bunge ni watu wazima mno kiumri na wengine wameshachoka sana kifikra kwa hiyo kuna hatari ya kupitishiwa katiba kandamizi ambayo itatubana kwa miongo kadhaa wakati huo huo walioipitisha wakiwa makaburini!
 
Profesa Shivji anatengenezewa Katiba na Kina Lema, Bulembo,Jah People, Joseph Ngonyani ( Maji marefu). Kama tumechagua kuwa Wajinga hakuna mwenye ubavu wa kutufanya Werevu.
 
Then anazungumzia mabilioni ya uswisi eti bado wapo kwenye upelelezi,ila kuna sehemu wakifika wanakwama,hivi ni nani mjinga unaye mdanganya serikali ya uswisi,usa,uk,wakitaka reference yoyote tanzania hamtowapa?kweli kweli mnakwama labda hamkwami kwa wazungu ambao nawajua mimi,they very smart hawawezi kusupport ufisadi
 
Huyu hajitambui.

Kwa AG asiyefahamu umuhimu wa katiba mpya baada ya miaka 50 ya taifa mpaka aonyeshwe njia na boss wake, kwa AG asiyefahamu nini kinaendelea katika operation zilizochini ya serikali yake(ref. OTU) na AG anayeonyesha mfano mbaya bungeni kwa kauli zisizo na staha basi Prof. Shivji na Dk. Bana ni makini mara 1000 zaidi ya ndugu yetu Fredrick Werema.
 
Back
Top Bottom