FREE ADVICE kwa WANAOTAFUTA KAZI

cosM

Senior Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
194
Reaction score
124
Habari wana JamiiForums, natumaini kwamba ni wazima wa afya. Napanda jukwaani kwa msukumo nilioupata ndani yangu kuwafikishia ujumbe rafiki zangu, vijana wenzangu.
Mimi ni kijana mwenzenu nimemaliza CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) mwaka huu 2013.

Kiukweli nafasi za kazi ni chache sana kulinganisha na idadi ya Wanafunzi wanaohitimu na wale ambao wako sokoni wakitafuta ajira hivyo kusababisha kukithiri kwa rushwa, kujuana na Mambo ya kindugu ndugu. (mtoto wa mjomba, Shangazi, mtoto wa rafiki yake bibi na kadharika) hivyo inafanya nafasi za ajira kuwa ngumu kupatikana hata ikipatikana ni kwa bahati na na kushikana mashati.

Kuna msemo wa kiswahili unasema '' dhahabu hata ikifukiwa kwenye Mchanga, vumbi zito, hata ikitupwa jalalani itangara tu" pia mafanikio ya Mtu huwezi kuyazuia kuja hata Kama asipo fanikiwa Leo atafanikiwa kesho, lakini pia kufanikiwa kwa Mtu inategemeana na Mambo mengi kutoka kwa Mtu mwenyewe.
Siku zote Kama ni mtafutaji wa Kweli changamkia *FURSA* ukifanya hivyo mara nyingi uwezavyo *BAHATI NA MAFANIKIO YANAKUFUATA NYUMA YAKO *

Unaweza kujiuliza Kwanini naandika uzi mrefu kiasi hiki?
First of all I want to witness what has happened to me and also to freely pass advice to friends.

" Luck is quite predictable, if you want more luck take more chances, be more active, show up, be flexible and present yourself "

Mimi nimetoka kijijini huko DODOMA, mimi ni wa kwanza kwenye familia yangu kufika chuo KIKUU, hivyo sikuwa na connections wala kumfahamu Mtu yeyote ambaye angenisaidia kupata kazi, hivyo ilibidi nijiongeze sana, mara nilipomaliza chuo nilikutana na marafiki wa Kweli na WANAFIKI ambao siku zote tulipokua tukipiga story walikuwa wananikatisha tamaa kuhusu swala la kupata ajira, na ilikua inasababisha kesho yangu ikawa inafifia, ila nashukuru baba yangu alinitia moyo akasema usikate tamaa wala kuvunjwa moyo na wapumbavu hata usipopata ajira mwaka huu hata 2019 utapata tu Usijali ila alinisisitiza nijishughulishe na kazi za kawaida angalau nipate pesa ya kuunga Internet bundles na kuni keep busy ili nisije nikachanganyikiwa kwasababu vijana wenzangu niliowaacha kijijini wako mbali kimaisha wame fanikiwa kupitia biashara na kilimo.
ILA PIA RAFIKI YANGU WA KWELI AKANIAMBIA..." Usijali best, usikate tamaa HARD WORK PAYS "

Nilikua na matokeo mazuri na yakuvutia kuanzia shule ya msingi mpaka chuo pia ninaweza kuyatetea.

Nashukuru mwezi uliofuatia nilipata kazi katika kampuni kubwa hapa Tanzania, SIKUWA NA MTU WA KUNIUNGANISHA WALA NINI.
Kwanini nimesema hivyo? Fanya yafuatayo, WALK YOUR DREAMS TO REACH YOUR DESIRED FUTURE, it is possible, everything lies into your hands.

1. USIJIFUNZE KWA WALIOSHINDWA
Kiukweli Watu walioshindwa wanamaneno mengi pia wanakatisha tamaa na unaweza kujikuta uko nje ya reli

2. BE CONFIDENT THAT YOU CAN.
Mkumbuke rose muhando" Woga wako ndio umasikini wako " be confident, show up and really present yourself, deliver to your best level to convince interviewers.

3. LEARN HOW TO EASILY MAKE FRIENDS, GET CONNECTED TO PROFESSIONAL NETWORKS AND MEET PEOPLE OF YOUR KIND sign up to professional networks like Linked in and the like.
Mimi binafsi linked in imenikutanisha na Watu wengi ambao wame kuwa msaada mkubwa sana kwangu. Sasa ukimaliza kusoma huu uzi create account sasa hivi ili utengeneze network ya marafiki

4. ACHA DHAMBI WAKATI UNAFANYA MAOMBI YA KAZI
Inawezekana ukawa umefanya vizuri sana presentation kwenye interview pia wakawa wameamua kukuajiri cha kushangaza hupewi hiyo nafasi na kupewa Mtu mwingine, Inawezekana jina lako limeandikwa katika majina ya miongoni mwa waajiriwa wapya ila Mwisho wa siku jina halipo limeandikwa la mwingine, hii inaweza kutokea kwa ajili ya DHAMBI iliyo fanya.

5. Usikate tamaa, ongeza juhudi katika kile unachokifanya kutimiza ndoto zako." DON'T LOOK WHERE YOU FELL INSTEAD CLOSELY LOOK AT WHERE YOU SLIPED " work on your weaknesses to make it happen.

6. Kitu kibaya kuliko vyote USIJITENGE NA JAMII KISA UMESOMA HADI CHUO KIKUU, kumbuka mchango wa jamii kwako kwa namna moja au nyingine, najua kuna Watu wanasema Kwani hao Watu wananilipia Ada? Na fanya niwezalo. Hapana tena umekosea sana ukisema hivyo Jamii inakudai deni kubwa sana hata kulipa huwezi. Hata Kama Wewe ni billionaire huwezi kulipa deni ambalo unadaiwa na jamii.

7. USIJIFANYE MJUAJI
usikurupuke, usiropoke, jifunze kusikiliza kisha cheza na mind zao.

8. MWISHO KABISA, KUMBUKA KUJIANDAA KABLA HUJAENDA INTERVIEW, LAKINI USI COMPLICATE KATIKA SWALA LA MAVAZI YA INTERVIEW MAANA unaweza UkAWACHUKIZA NANAOKU INTERVIEW HII INATOKEA PALE UNAPOKUA UMEPENDEZA KULIKO WENYEWE.
NOTE : KABLA HUJAINGIA CHUMBA CHA INTERVIEW BE FRIENDLY AND FLEXIBLE, ONGEA NA WENZAKO MLIOKUTANA KWENYE INTERVIEW PIA USISAHAU KUCHUKUA MAWASILIANO YAO.

ASANTENI sana.

Best regards
CosM
 
dah! Umenifumbua sana macho mzazi ubalikiwe na kazi njema
 
Binadamu wakiona una mafanikio watakukatisha tamaa songa mbele usigeuke nyumba ndio dunia mie najua umetoka mbali king kong sio wote watakupendaa,TENDA MEMA USINGOJE SHUKRANI CHEKA NA WATU WOTE COSYM
 
Binadamu wakiona una mafanikio watakukatisha tamaa songa mbele usigeuke nyumba ndio dunia mie najua umetoka mbali king kong sio wote watakupendaa,TENDA MEMA USINGOJE SHUKRANI CHEKA NA WATU WOTE COSYM

Pamoja sana King Kong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…