Free baggage allowance - azam marine??

Akthoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2007
Posts
1,001
Reaction score
1,021
Wapendwa JF, SUMATRA & UONGOZI WA AZAM MARINE.


Naomba kufahamishwa ni kiasi gani cha mzigo kinachoruhusiwa kama "free baggage allowance" unaposafiri na Boti za Azam(Coastal Fast Ferries).

Jana nilitozwa kiasi cha Tsh. 7000 kwa risiti na 72638 pale Bandari ya Zanzibar kulipia kiasi cha kilo 35 za tambi (Maandalizi ya Futari ,Mwezi mtukufu wa Ramadhali). Tulisafiri na Boti ya Kilimanjaro 2. Kuna jamaa anafahamika kwa jina la Mchina ndiye aliyekuwa anasimamia zoezi hilo; nilibishana nae sana ili kujua haki yangu lakini hatimae nilikulibali kulipa kiasi hicho kwa shingo upande. Tafadhalini tusaidiane kujua haki za wasafiri kwani ikiwa hatujui basi watu wengi watakuwa wanaibiwa na kudhulumiwa kila siku; Hata nilipo angalia kwenye tiketi ya safari hapakutajwa uzito/ ujazo wa kusafiri nao bila kulipia. Nawasilisha kwa wajuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…