Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kuelekea uchaguzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, chadema ngazi ya taifa,
Yapo mambo mengi sana yametokea na yanaendelea kutukokea kwa nyakati tofauti, na mengi yakihusiana na joto la uchaguzi wa chama hicho, January 22,2025.
Kwa upande wa Freeman Aikaeli Mbowe,
hali hii itamsaidia sana katika kupanga vizuri safu ya uongozi wa Chadema ngazi mbalimbali nchini kwa miaka mitano ijayo, na hata kutambua uaminifu wa mrithi wake katika wakati muafaka atakapojiridhisha kung'atuka na kumuachia mwingine mikoba ya kuiongoza Chadema.
Pamoja na hayo,
Freeman Aikaeli Mbowe anapata fursa ya kujua na kujifunza watu wema na wenye hila dhidi yake na uongozi wake. Na hapo atapata fursa na nguvu mpya iliyoambatana na umakini mkubwa katika kufanya kazi za chama na aina mbalimbali za watu wanaomzunguka.
Ndugu Mbowe,
atapata pia fursa na wasaa muhimu sana wa kuelewa vyema marafiki wa kweli na watu wanafiki waliopata kuapa mbele ya kadambasi kwamba hawatathubutu kushindana nae hususani kwenye kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama, kwa madai ya heshima na udugu wa kifamilia walioujenga kwa muda mrefu sana na kwa uaminifu mkubwa.
Atajiridhisha kwa kuona mchana kweupe unafiki wa kiwango cha juu kwa baadhi ya wanachadema vibwengo na misukule wakiikimbia chadema baada ya kushikishwa adabu na wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa.
Chadema national chairman in waiting,
Freeman Aikaeli Mbowe,
atajiridhisha pasina shaka idadi ya maadui, vibwengo na misukule wa kisiasa alionao ndani ya Chadema na hatimae kwenda nao sambamba, bampa to bampa katika kufundishana siasa na kushikishana adabu katika siasa ili iwe fundisho na pawepo heshima siku zijazo.
Jambo la mwisho la muhimu zaidi, chairman Mbowe atawabaini rasmi wasaliti wake,
Lakini jambo zuri zaidi atawabaini viongozi wenye maono na uelekeo moja pamoja nae na atawajua wanachama watiifu kwake na waaminifu kwa Chadema kwa ujumla, na hiyo itakua fursa nzuri kwake kuisuka na kuiunda Chadema mpya, yenye sura na vipaumbele vipya na muhimu kwa maslahi na mustakabali wa uhai na ustawi wa chadema kitaifa.
Shukrani za kipekee sana ziwaendee wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa, wakiongozwa na wenyeviti wa kanda, mikoa, wilaya na kata nchi nzima, kwa namna walivyo simama imara kwenye nafasi zao
Mungu Ibarki Tanzania 🐒