Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) amejibu kauli ya Rais Samia kuwa 'Kifo ni Kifo tu' amesema
"Ni kweli vifo vipo vingi na watu wengi wanapoteza maisha, tunakubali, lakini maisha yote haya yanayopotea kila mmoja una thamani yake ya kipekee hasa pale mtu 'anapodakwa na vyombo vya dola', halafu anapotezwa, na ndiyo sababu tunasema kama basi tuna wasiwasi na mambo kama hayo ili tutengeneze mazingira ya kulifanya taifa letu liwe na mshikamano, tupate vyombo huru vinavyoweza kufanya uchunguzi ili yeyote miongoni mwetu asiwe ni mchezaji na refarii, ninaamini ni rai ambayo sisi tuliitoa kama chama (CHADEMA) tukijua ni nia njema tu ambayo hatutalaumiana kwa sababu anayechunguza ataweza kuyaweka mambo wazi ili wale wanaohusika katika kufanya makosa haya wachukuliwe hatua za msingi, bado tunaendelea kusubiri lakini hatutarudi nyuma katika kusimama kutetea ukweli na haki katika taifa hili"
"Na ninawaomba washiriki wote wa kongamano hili {Mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)}, kama tunataka kuliponya taifa letu kwa mtazamo wa muda mrefu, lazima tuwe na ujasiri wa kusimama na kusema ukweli, leo tunajadili hali ya demokrasia Tanzania ambayo tumedumu nayo kwa miaka 30, kweli kuna maendeleo kidogo tumefanya, lakini kama kungekuwa na dhamira za kutosha za kisiasa kwa makundi yote hasa wale wenzetu ambao wamepewa dhamana ya kuliongoza taifa, Tanzania leo tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana, hatujaweza kufaidi matunda ya demokrasia kwasababu tumelumbana kwa muda mrefu bila sababu"