Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa kweli, this is the right way ku - deal na mtu huyu......

Na kwa ujumla mtu mwenye akili timamu anashindwa kumwekewa mchungaji huyu kuwa amepagawa na pepo la namna gani.....

Bila shaka hata huko CCM wanapata shida sana kumwelewa huyu mchungaji wa Kanisa anapokuwa anafyatua mdomo wake. Ma - CCM yameshajua ni tapeli fulani kama yule Mkongo - Kiboko cha wachawi.....

Haiwezekani kwa mtu mwenye maadili ya uchungaji wa Kanisa awe mzushi na muongo wa wazi kiasi hiki huku akiwa na uso mkavu kabisa anapokuwa anaoayuka udanganyifu wake...
 
Mbona hizi fidia ni kama zinatajwa tu kwenye mahakama lkn hazilipwi?

1. Bilioni 5 the late Membe toka kwa Musiba ....kimya.
2. Bilioni 5 za Masoud Kipanya toka kwa Mwijaku.....kimya.
3. Na sasa ni bilioni 5 za Mbowe toka kwa Msigwa.....
Kwani ulitaka wakilipwa wakujulishe?
 
Sasa kutajwa na msigwa tu alipwe bil5 siku akiwa rais huyo mbowe wenu wananchi si tutalipishwasana hozo bil5? Ina maana mbowe na wafuasi wenu hamna political tolerance?
Kumbe kuukubali uongo ni "political tolerance"!!??
 
Yeye ni kiongozi wa umma kama hataki kuitwa mwizi wakati kweli chama kinapokea ruzuku lakini hata ofisi hakina achane na siasa akakoroge mbege machame
Mbona yeye anamuita Samia mwizi?
Kama anamwita Samia mwizi na si mwizi kweli, basi Samia anayo haki na kila sababu ya kwenda mahakamani ili kudai jina lake lisafishwe, lakini kama hajaenda mahakamani, haimaanishi mwingine akiitwa mwizi wakati si kweli, asiende mahakamani.
 
Ulikisoma ulichokiandika na kukielewa kweli kabla ya kutuletea JF!!??
 
Mahakama inaenda kusikiliza madai ya Mwenyekiti kwamba amechafuliwa.

Hoja za msigwa zinapaswa kujibiwa na chama kupitia katibu mkuu kama ambavyo Lissu alipendekeza.
Ushahidi wa kuwa madai ya Msigwa ni uongo si utatolewa na upande wa Mbowe (KM Mnyika ataitwa kama shahidi), au ushahidi wa madai ya Msigwa kuwa ni kweli utatolewa na Msigwa (hapa napo KM Mnyika anaweza kuitwa kama shahidi kuthibitisha madai ya Msigwa kama ni kweli ama la, ndipo vielelezo vya ukweli au uongo kuwekwa hadharani na mwisho wa siku hoja zake Msigwa zinakuwa zimejibiwa mbele ya chombo ambacho uongo ni kosa kisheria).
 
Lissu aliomba hoja za msigwa zijibiwe kabla hata ya sakata hili la kupelekana mahakamani, lakini Mnyika na ofisi yake hawakufanya hivyo.

Ngoja tuone labda huko mahakamani panaweza kuwa sehemu sahihi ya kumaliza utata huu.
 
Lissu aliomba hoja za msigwa zijibiwe kabla hata ya sakata hili la kupelekana mahakamani, lakini Mnyika na ofisi yake hawakufanya hivyo.

Ngoja tuone labda huko mahakamani panaweza kuwa sehemu sahihi ya kumaliza utata huu.
Kesi tamu sana hii, UTABIRI, ITAPELEKEA ANGUKO LA MWENYEKITI, STAY TUNES!
 
Huyu dingi ana matatizo
Anaropoka sana
Anatakiwa anyooshwe haswa
Hilo jopo la mawakili naomba mumnyooshe hii kenge
 
Imeandikwa kitaalamu kabisa.
 
Lissu aliomba hoja za msigwa zijibiwe kabla hata ya sakata hili la kupelekana mahakamani, lakini Mnyika na ofisi yake hawakufanya hivyo.

Ngoja tuone labda huko mahakamani panaweza kuwa sehemu sahihi ya kumaliza utata huu.
Mnyika na ofisi yake wanawajibika kujibu hoja zinazoelekezwa CHADEMA tu na si kwa mtu binafsi - tena kwa utaratibu rasmi wa kiutendaji, si kwenye majukwaa ya kisiasa. Itakuwa kituko Mnyika akikurupuka kuja hadharani na mafaili ya chama kujibu porojo zinazoenezwa na Msigwa mitaani kumhusu Mbowe. Katibu Mkuu makini wa chama kikuu cha upinzani hawezi kuwa zoba kiasi hicho.

Msigwa kamsema Mbowe, hivyo Mbowe ndiye mjibu hoja. Na ndio keshajibu hivyo kwa kudai msamaha au Bilioni 5, period. Anasubiri majibu ya Msigwa.
 
Mbowe kama kuambiwa ukweli kidogo tu anakimbilia mahakamani badala ajibu hoja na kujisafisha je siku akiwa Rais ataweza kuvumilia maneno? Au ndo atapeleka kila mwananchi mahakamani na ikiwezekana kuwa mtekaji pia
Sasa si ukweli utajulikana mahakamani mara hii mnasema Mbowe akiwa rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…