SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Kamuulize mwenyewe sisi hatuna jibu.Je, Tundu AM Lissu kama Mwanasheria nguli kwenye nchi Yuko tayari kuona rafiki yake kipenzi Cde Peter Msigwa akiozea jela kwani ni kweli hana uwezo wa kulipa hiyo 5bln.
Kwa hili allegation alizozitoa against Mbowe, lazima zimkaange kisawasawa! Hii siyo siasa kuwa pesa za Join the chain aliziiba kwenye akaunti yake,. Kuna maneno ya kisiasa ambayo unaweza kuyasema kisiasa kuwa ni mbwembwe za kuijnadi, lakini siyo ya kuwa huyu ni mwizi, msherati, mfiraji halafu sijui ujitetee kuwa ni siasa za majukwaani.Akiwa Chadema huyu Mchungaji Msigwa ndio alikuwa akiongoza mashambulizi ya Uzushi dhidi ya Hayati Lowassa na Mzee Kinana
Mchungaji Msigwa alijidanganya sana kudhani Mbowe ataukalia kimya uzushi na Uwongo wake
Katika hili ndipo CCM watakaa kando kabisa, hilo Nina uhakika nalo
Jumaa Mubarak 😀
Ni mchungajiNinani huyo msigwa
😀😀Tundu Lisu: Mchungaji Msigwa alikuwa rafiki yangu alipokuwa vitani nasi sasa amesalimu Amri kwa adui Urafiki Wetu umekwisha
Jumaa Mubarak 😀😀🌹
CCM wamsaidie Msigwa kumlipa Mbowe hiyo 5bn mara moja pesa wanazo.1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake
My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!
=====
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi na kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.
“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.
Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”
Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).
“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.
Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.
“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.
Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Pia soma
- Freeman Mbowe amdai Mchungaji Peter Msigwa bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafulia jina lake
- Peter Msigwa: Msajili wachunguze CHADEMA, wana vikundi vinaitwa ZOO na JOB. Mbowe ni Nkurunziza
- Mchungaji Msigwa: Nitazunguka Nchi nzima kuelezea Uongo wa CHADEMA
- Mchungaji Msigwa: Mbowe siyo Msakata Rhumba maarufu ndio sababu hadi sasa bado yuko Jukwaani japo muda umeisha!
- Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini
- Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi
View attachment 3088476View attachment 3088473View attachment 3088474View attachment 3088475
akijiingiza huko amekwisha!Je, Tundu AM Lissu kama Mwanasheria nguli kwenye nchi hii,
Je, atakuwa tayari kuona rafiki yake kipenzi Cde Peter Msigwa akiozea jela?
Ni dhahiri Msigwa hana uwezo wa kulipa hiyo 5bln vinginevyo chama kimlipie.
kweli hizo kwao ni kitu kidogoCCM wamsaidie Msigwa kumlipa Mbowe hiyo 5bn mara moja pesa wanazo.
Kama ni Yule aliehamia ccm kwa mbwembwe , ccm si wamlipie hilo deni?Ni mchungaji
😀😀Ni mchungaji
Chawa mamakoHujajibu swali Muheshimiwa Chawa
Wanaomtuma , wanamsukumiza kwa mbowe😀😀Mkubwa tunaweza kuona chanzo cha habari yako kama hautajali?
By the way ni jambo jema kumtaka alipe hiyo fidia ama akathibitishe madai yake
Maana Mchungaji Msigwa Kila Siku yeye na Mbowe, Mbowe na yeye
Utasema wana ugomvi wa kuibiana mali ama Wapenzi 🙌
Tupe picha yake akiwa kashika biblia😀Ni mchungaji
Hapa hapa ndipo pahala sahihi PA wana chadema wenye maulizo na madukuduku yao tutapata maelezo ambayo hapo hawali ilikuwa ngumu sana kuhoji,, wapo viongozi ndani ya chadema tena waandamizi wanashindwa kuhoji, maana kuhoji tu, na hatari sana, hili la kutokuhoji linapelekea baadhi kwa siri wanakusudia kuhama chama.Panapo fuka moshi pameficha moto, na hapo hakuna nyasi, yaani hao wawili ndiyo watakao uzima moto kwa maana kwasasa wameuwasha. They have started, have to finish