MenukaJr
Member
- Apr 24, 2021
- 50
- 128
Freeman Aikael Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akiwa Arusha licha ya kutumia muda mwingi kumsimanga JPM, ambaye hawezi kujitetea tena amemjaribu Rais Samia Suluhu Hassan.
Freeman Mbowe amesema kuwa Chama chake hakitashiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa hadi pale itakapopatikana Katiba mpya. Amesisitiza, wanataka Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na hawatasubiri itokee kwa hiari isipokuwa wataidai, watapambana kuipata. Kwa maneno haya ya Freeman ni kwamba, Chama chake kitahakikisha Katiba mpya inapatikana kwa njia yoyote, iwe halali au haramu. Haya ndio mambo JPM alikua anakataa. Freeman Mbowe anamjaribu Rais Samia, anataka kujua ubavu wake katika kutumia mamlaka ya Urais.
Freeman Mbowe anamjaribu Rais kwa sababu zifuatazo;
MOJA Freeman Mbowe anafahamu kuwa Rais Samia amerithi uchumi mbovu wa nchi ulioathiriwa na janga la corona. Rais mwenyewe amerudia mara kadhaa kwamba mambo mengi katika nchi yetu hayawezi kufanyika kwa sababu ya mdororo wa uchumi uliofishwa na corona katika nchi yetu na Duniani kote. Kwa uchumi huu, hakuna Rais anaweza kuongeza agenda nyingine yenye kuhitaji pesa nyingi. Hiyo bajeti haiwezi kupatikana kwa sasa kama maneno ya Rais kuhusu hali ya uchumi ni ya kweli.
Kwa vyovyote vile kumtaka Rais aanzishe mchakato au aendeleze mchakato wa Katiba mpya katika uchumi wa namna hii ni kumjaribu. Watumishi watamshangaa ikiwa tumeshindwa kuwaongeza mishahara halafu tupeleke pesa nyingi kwenye jambo ambalo linaweza kufanyika wakati wowote.
PILI Freeman Mbowe anafahamu wazi kuwa Rais Samia Suluhu amerithi miradi mingi mikubwa yenye kugharimu pesa nyingi zaidi. Freeman anafahamu namna ambavyo Watanzania wanategemea miradi hii kukamilishwa kwa wakati kama ilivyokusudiwa. Rais mwenyewe amekiri hadharani kwamba atasimamia ukamilifu wa miradi hiyo kwa wakati. Katika nchi yenye kukamilisha miradi mingi, mikubwa yenye kutumia pesa nyingi kama hii, kumtaka Rais kuanzisha mradi mwingine wa Katiba mpya wenye kutaka pesa nyingi ni zaidi ya kumjaribu.
TATU Freeman Mbowe anafahamu kuwa Rais Samia Suluhu amebadilisha kidogo mfumo wa makusayo ya kodi katika nchi. Mfumo wa makusanyo ya kodi kwa sasa unatarajia kupunguza mapato ya nchi kwa kipindi fulani mbele. Kwa sababu hii, nchi haiwezii kuwa na mapato ya kutosha kufadhiri mambo mengi kwa mkupuo mmoja.
Tunahitaji kubana matumizi kuliko ilivyokuwa hapo awali ili nchi isitetereke. Hatuwezi kukopa pesa ughaibuni kwa ajili ya kutengeneza Katiba yetu kwa sababu mashart ya mikopo yanaweza kutupangia aina ya Katiba ya kutengeneza. Hii ni sababu nyingine ya wazi kwamba sharti la Freeman Mbowe kwa Rais Samia ni jaribu kubwa.
Ushauri kwa Rais Samia Suluhu Hassan:
1. Ni lazima ajitokeze kuonesha rangi yake. Wapinzani wasipoifahamu rangi yake wanaweza kumyumbisha. Wapinzani wa nchi hii hawana utulivu, wanaweza kuomba ukutane nao kuzungumza huku wakikutukana kwenye mikutano yao. Wanaweza kutaka hili leo, kesho lile; yote yasiyotekelezeka. Kwa vyovyote iwavyo wanahitaji kudhibitiwa, kuoneshwa mipaka.
2. Ni lazima Rais atoe msimamo wake mapema kuhusu Katiba mpya. Hiyo itasaidia kuinusuru nchi na hekaheka zisizo na msingi. Kama Rais anakubaliana na msimamo wa Katiba mpya tuanze mapema mchakato, kama hakubaliani nao tufunge mjadala. Tuna mambo mengi ya kufanya! Dalili zinaonesha tunaweza kuwa na nchi yenye maandamano ya kisiasa na mizozo isiyokwisha kama ilivyokuwa huko nyuma ikiwa hatukuchukua hatua mapema.
Asanteni!!
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.