Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CHADEMA Mikocheni amesema
Kwa mwaka huu (2024) na sehemu ya mwaka jana (2023), wako Watanzania zaidi ya 200 katika ukanda huu na nje ya ukanda huu, ndani ya kanda hii ya Pwani, ya Dar es Salaam na nje ya kanda hii ambao hawajulikani waliko, siyo hawa 80 walioripotiwa na TLS, zaidi ya watu 200 wamepotea.
Mambo haya ni mwendelezo wa maelekezo ya viongozi wa serikali ambao huko nyuma walipata kusema shughulikeni nao yaani kwamba sasa yawezekana baadhi ya watu wamepotezwa walikuwa na jinai zinazowahusu, inawezekana, lakini hakuna jinai kwa sheria na katiba ya nchi yetu inayoruhusu vyombo vya dola kuhukumu mtu kwa jinai aliyofanya bila kumfikisha kwenye mahakama za nchi yetu.
Kwa hiyo hakuwezi kuwa kisingizio chochote kwamba huyu tuliyemshughulikia ni Panya road au ni mwizi, hakuna uhalalishaji huo, hata mwizi anapaswa kupelekwa kwenye vyombo vya sheria katika nchi yetu.