Freeman Mbowe Kuwatunuku Vyeti leo wahitimu wa CHASO vyuo vikuu mkoani Kilimanjanro.

MWANAKASULU

Senior Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
197
Reaction score
71
Leo J2 tar. 2/06/2013.saa sita na nusu Mchana katika ukumbi wa Hindu Mandal ulioko Moshi mjini Opposite na stand kuu ya Mabasi kutakuwepo na Mahafali ya wahitimu wa CHADEMA STUDEMA STUDENTS ORGANIZATION(CHASO).-mkoani Kilimanjaro.

Mgeni Rasmi ni Freeman Mbowe ataongozana na Mwenyekiti wa Bavicha John Heche, Katibu wa vijana Deogratius Munish, Jembe la Arusha Mjini G.Lema,Jembe la Arumeru Mashariki J.Nassari maarufu kama Dogo Janja,Jembe la Moshi Mjini kamanda F.Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa na Waheshimiwa madiwani wote wa Moshi watakuwepo ndani ya nyumba.

Wahitimu watakao tunukiwa vyeti ni makamanda 205 kutoka vyuo vikuu 6 vilivyoko mkoani Kilimanjaro yaani KCMC,MUCCoBS,SMUCO compus zote ,MASOKA pamoja na Mwenge University.Lakini chuo kilichotoa wahitimu wengi kuliko vyote ni Mwenge University kilichotoa wahitimu 102.Shamlashamla ni kubwa sana kila kona ya vyuo tajwa na wanachi wote walioko ndani na nje ya mji wa Moshi wamekaribishwa kushuhudia tukio litakalo dumu kwa masaa 5.

''Mabadiliko yako mikononi mwako na Wewe ni sehemu ya Mabadiliko''.(Mahtima Gandhi).HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
 
Nini implications ya hivi vyeti?

Jiulize kwanza nini maana ya vyeti au cheti.Pia jiulize ni vyeti vingapi umewahi kutunukiwa na kwa nini umetunukiwa ni kweli kila mmoja alistahili kutunukiwa kama ulivyotunukiwa.Na kama hujawahi kutunukiwa cheti chochote basi tafuta waliotunukiwa cheti chochote kile umuulize kwa nini unatunukiwa cheti?

Na kina maana gani? Kama umebahatika kufika shule na kama ni muumini wa dini lolote umewahi kupewa cheti kinachoonesha ulikuwa active member wa dini gani si hilo tu nina hakika umebahatika kuwa na cheti cha darasa la saba au f4 au f6 au level yoyote.vilevile kwenye taasisi mbalimbali umewahi kushuhudia watu wanapewa vyeti sasa kama una cheti kati ha hivyo vyote jiule mwenyewe vina Implications gani?

Ndipo utaelewa kwa nn makamanda wa CHASO wanatunukiwa vyeti.
 
Go ahead CHADEMA, kwan vijana taifa la leo.
 
Next time mwa dress hivi .. MHESHIMIWA Freeman Mbowe.....
 
Mpaka sasa nipo Hindu Mandal hall bado vijana wajisogeza taratibu
 
Hongereni sana wana CHASO mkoa wa Kilimanjaro, nafurahi kusikia bado mmeendelea kuwa wamoja bila kujalisha vikwazo vinavyo wakabili.
 
Baada ya utambulisho Meya wa Manispaa ya moshi ndo anahutubia sasa. Anawaasa vijana kuienzi kazi iliyofanywa na wazee wetu. Anawaasa wasikubali kurubuniwa.
 
Nami nimefika Ukumbi wa Hindu Mandal kuungana na Makamanda wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro.
Mambo yako vizuri hadi raha.

CHADEMA YATOSHA!!!!
 
Naona wapo uwanja wa nyumbani.
 
Mpaka sasa viti vyote vilivyoandaliwa vimejaa, na kuna makamanda wengi sana wamesimama nyuma na Wengine tumekaa sakafuni pembezoni(mimi ni mmoja wapo) kwa sababu ya kukosa viti.
Please wahusika tunaomba mlete viti au mabenchi chap chap tuweze kukaa vizuri.

UPDATES
Kwa sasa kiongozi (mwenyekiti?) wa CHASO mkoa wa kilimanjaro anatoa hotuba/Risala.
 
*TAARIFA
1/Hakuna mtu yoyote aliyeletwa kwa kubebwa kuja kuhudhuria mahafali haya.

2/Hakuna mtu yoyote aliyepewa posho kama motisha kuja kuhudhuria.

3/Hakuna motisha ya vinywaji, chakula wala burudani ya wasanii iliyotolewa kwenye mahafari haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…