Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
"Mna tabia ya kufikiri Wakenya wana akili sana, Wakenya hawana akili yoyote ya maana kuliko Watanzania ila tofauti yao na sisi wale walifundishwa Kiingereza tangu chekechea kwahiyo ukienda kwenye mabenki yetu, mahoteli ya mbuga za wanyama huko wameajiri Wakenya kwa sababu waliandaliwa kushindana kwenye soko la ajira la kimataifa," - @freemanmbowetz Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
"Viongozi wanawaambia Watanzania wa kawaida Kiswahili ni lugha nzuri sana endeleeni kusoma Kiswahili tuenzi lugha ya Taifa ni sawa wala sisi hatupingi lakini ambacho @chadematzofficial tunatofautiana na CCM ni huu ubaguzi wa elimu, tunasema watoto wetu hawa ni lazima tuwape elimu ambayo wanaweza wakashindana na watoto wengine wowote duniani, ili watoto hawa waweze kushindana kwenye soko la ajira la dunia ni lazima wafundishwe elimu zenye lugha za kimataifa," - @freemanmbowetz Mwenyekiti wa CHADEMA
#CHADEMAArusha