Freeman Mbowe lazima afungwe ili Uhuru wa kweli upatikane

Freeman Mbowe lazima afungwe ili Uhuru wa kweli upatikane

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
1,864
Reaction score
5,695
Huu sio wakati wa kumlilia Mbowe Wala sio wakati wa kuwalaani CCM. Ili Uhuru wa bandia wa akina Kingai na Mahita wa kuteka, kutesa na kuua raia wema Kama akina Moses Lijenje na wengineo uondoke ni lazima Mbowe afungwe na sio Mbowe tuu na wale wote wazalendo wa kweli wapite katika tanuru la Moto Kama alivyo pita Tundu Lissu na wabakie kuwa waaminifu hata kufa.

CCM hawaleti Mateso hayo kwa hiari yao bali wanalazimishwa na wakati uliopo. Hiki ndicho kipindi cha mwisho kwao kutupa kete ya mwisho ya kupigania uhai wa matumbo yao. Wamejaribu kete ya vitisho ikabumba, wakajaribu kete ya bunduki ikabumba Sasa kete yao ya mwisho ni kufunga wapinzani. Kama ulisoma kile kitabu cha profesa Rostow akielezea hatua zinazotakiwa kufuatwa kufikia maendeleo ya kweli, hatua ya kisiasa tuliyopo Sasa Tanganyika ni ile hatua ya nne kabla ya mwisho akiita "Drive to Maturity.

Mbowe akifungwa ni faida kwa nchi na ni hasara kwa CCM. Watu wakifumbuliwa macho kuwa hawapo huru kiuchumi, kisiasa kijamii na kiutawala huwa raia wazuri Sana. Hii ni fursa kubwa kwa Chadema sasa kutumia jukwaa la kisiasa la ndani ya nchi hii na kimataifa.

Naiona Chadema inaenda kuwa Chama kikubwa na kinacho kubalika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sifa ya kujali utu demokrasia na haki za Binadamu. Hata maandiko yanasema mkipigwa kwa ajili haki shangilieni kwakuwa thawabu yenu ni kubwa na imeandikwa mbinguni.

Huu ndio wakati wa kutenganisha maji na mafuta. Wakati wa kujua vyama halisi vya siasa vya upinzani na na vile vyama vya upinzani vikiwa ni CCMB. Ni wakati wa kujua mashirika halisi ya kutetea Haki za Binadamu na Yale ya kutetea matumbo yao. Ni wakati wa kujua viongozi halisi wa Dini ya Mungu wa kweli na viongozi wa Dini halisi wa shetani.

Kule Msumbiji na Afrika kusini sifa moja wapo ya mgombea urais inayo muongezea Imani kwa wapiga kura ni kuwa alishiriki kikamailifu ktk vita vya ukombozi wa nchi hiyo akiwa vitani ndani ya nchi hiyo au wakiwa nje ya nchi. Fuatilia viongozi wote wa Msumbiji na Afrika kusini utagundua walikuwa sehemu ya mapambano dhidi ya Uhuru wa kilaghai wa akina Kingai na Mahita nchini mwao. Hii itaenda kutokea hata Tanzania. Chadema inaenda kushika dola na kumuondoa mkoloni mweusi CCM.

Makaburu hawakumfunga Mandela kwa hiari yao. Hoja zake zilikuwa hazijibiki hata ukitumia bunduki au Mateso, kuteka na kupoteza watu. Waliona kete yao ya mwisho ni tumfunge tu gerezani. Dunia ikapiga kelele wakati huo tukiwa shule ya msingi tukawa tunaimba nyimbo za kushinikiza Mandela aachiwe huru tukiwa tunakimbia mchaka mchaka.

Japo Mandela tulikuwa hatumjui lakini uzalendo wake kwa nchi yake ilitufanya tumuimbe. Hilo ndilo taifa ambalo Nyerere alijaribu kulijenga linalo jali utu wa watu wengine. Mandela mpya anaenda kuzaliwa Tanganyika na Dunia itampigania tukishirikiana na wazalendo wa nchi hii na kila aina ya silaha nawahakikishia itatumika kumlenga adui CCM.

Hii teua teua ya viongozi kutoka Chadema mnayo iona sio bure, ni uhalisia wa Mambo kuwa Chadema inakubalika na wananchi wote hata ndani ya CCM wenyewe. Huko Mbele tunako enda CCM itakuwa imekufa rasmi itakuwa ni vigumu mtu kuwa kiongozi Kama hakuwa mwana Chadema au hakuwa sehemu ya mapambano ya kudai Uhuru toka kwa mkoloni mweusi CCM.
Maendeleo hayana Chama.
 
Huu ni ukweli ambao wenye madaraka wametiwa upofu wasiuone(wamenyimwa maarifa ili waanguke) na ndio maana mnaona mtu anapewa promotion katika ya kesi tena kesi sensitive yenye sura ya kisiasa (kukosa/kunyimwa maarifa-Mungu ana makusudi kwa kila jambo).

Ummewaza kama ulivyowaza, hivyo leo hii umeniongezea imani kwa nilichokiwaza na kukiamini .

Ni kanuni za asili za kiulimwengu kwamba, wakati mwingone, inabidi watu au mtu fulani aumie ili kuokoa au kuponya wengine(kina Mandela na wengineo ni mifano mizuri tu).

Ukiwa muumini mzuri wa historia na maandiko matakatifu, unaweza kutafsiri matendo haya na baddae ukaonekana kama nabii mbele za watu. Ukweli ni kwamba, katika dunia hii iliyo-exist kwa mamilion ya miaka, hakuna jipya linalotokea likakosa reference ya matukio tangu enzi na enzi.

Kama nilivyowahi kusema huko nyuma, kipya katika dunia ya leo ni tekonolojia tu mengine yote ni marudio katika nyakati tulizonazo.

Narudia, Mungu ana makusudi kwa kila jambo na tutaona kusudio hill lkitimia.
 
Huo ni ukweli.kuna kikundi cha watu kinakaribia kufa kifo cha asili kwahiyo kinaona kila mwenye kutaka kuimarika zaidi yao ni mkosefu.Wasome alama za nyakati.muda haupo upande wao ata wafanyeje.
 
Uzi ulioenda shule, hongera sana, ili uhuru wa kweli upatikane wale wote wanaodhaniwa ni magaidi wafungwe kuwafurahisha CCM.
 
Wakimfunga ndo wataharibu zaidi, siku akitoka mtaa hautakalika kwa nderemo.
Hata hapa ilipofikia, wanashindwa wafanye nini. Kwa sababu wakifuta kesi, nchi italipuka kwa shangwe, wakimfunga, nchi itazizima. Namna zote mbili ni shida tupu. Hii wameiacha imesogea mbali mno, sababu ni kukosa washauri wazuri.
 
Kiroho statement yako ipo sahihi ila kimwili inagoma, Mbowe ana maisha pia at his @60. Hakuna njia nyingine ya kulikomboa Taifa kutoka hawa wakandamizaji zaidi ya hii.
 
Back
Top Bottom