Freeman Mbowe lazima afungwe ili Uhuru wa kweli upatikane

Tupo kwenye kipindi cha udhalimu lakini utapita tu.
 
Kiroho statement yako ipo sahihi ila kimwili inagoma, Mbowe ana maisha pia at his @60. Hakuna njia nyingine ya kulikomboa Taifa kutoka hawa wakandamizaji zaidi ya hii.
Hapo umetumia falsafa kuona ktk maumivu anayopitia Mbowe Kuna mwanga Mbele unakuja,huwezi kuona hayo kwa akilili za Kingai ngai tuu.
NOTE: Kingai ngai=ujinga
 
Kufungwa kwa Mbowe kumeshapangwa, lakini hali hii litaleta mabadiliko makubwa ndani ya Chadema. Naiona Chadema ikiangukia kwenye mikono ya vijana wenye msimamo tofauti na wasiokuwa na subira kama Mbowe. Ole wa amani ya nchi yetu maana wosia wa Nyerere kuwa Tanzania tusijione kisiwa umepuuzwa na wenye hati miliki ya taifa hili.
 
Wakati ni mwalimu mzuri, hata wale Makaburu wa Afrika kusini au Wareno kule Msumbiji hawakuwaza kuwa Tanzania itakuwa kituo Cha kunoa wapigania uhuru.
Nakuhakishia kikinuka CCM haifui dafu hata wiki moja tuu ya mapambano. Wapo watu ndani ya mfumo huu dharimu wanatafuta wapi kwa kutokea ili inchi ipumue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…