Fresh mixed salad/extended kachumbari

Fresh mixed salad/extended kachumbari

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
3,211
Reaction score
993
FRESH MIXED SALAD
Fresh (tamka; freshi) ni kitu kipya moja kwa moja toka shambani (yaani hakijapikwa), Wakati MIXED (tamka; miksidi) ni mchanganyiko wa vitu mbalimbali na Salad (tamka; saladi) ni kisindikizio, ni mbogamboga ama mchanganyiko wa mbogamboga na vitu vingine kama nyama, samaki nk .

Kwa lugha nyepesi, fresh mixed salad waweza kuiita ni kachumbari, lakini si kachumbari kwakuwa ina vitu vingi zaidi ya vile vinavyoingia kwenye kachumbari, pia kachumbari ni pishi la Kiswahili (ingawa inajulkana sasa sehemu nyingi duniani) wakati salad ni pishi la kizungu zaidi. Nadhani inatosha.

MAHITAJI:

[Show as slideshow]





























Utahitaji mboga mboga fresh zifuatazo, si lazima uwe nazo zote lakini walau zifikie 5;

  • · Nyanya fresh
  • · Vitunguu maji
  • · Pilipili hoho
  • · Kabeji
  • · Lettuce (tamka letusi)
  • · Maharage machanga (greenbeans (tamka; grinibinzi))
  • · Kaloti
  • · Rocket/ruccolla (tamka; roketi au rukola)
  • · Ndimu/limau fresh
  • · Chumvi
  • · Mafuta ya zaituni (Olive oil) vijiko 2 au 3.
INAVYOANDALIWA HATUA KWA HATUA:
1. Osha vizuri mboga mboga zote katika maji mengi yanayotiririka.

2. Kwenye mahitaji yetu kuna mboga mboga inaitwa maharage machanga/greenbeans, haya ni vigumu kidogo kuyala moja kwa moja mabichi; utatakiwa kisha kuyaosha ondoa miishio yake pande zote mbili huku huku na ukate katikati kila harage kupata vipande viwili na uyachemshe kidogo katika maji au unaweza kuchamsha maji vya kutosha kasha zima moto na utumbukize hayo maharage ndani yake kwa dakika kama 5 hivi kisha yachuje toka katika maji, hii inafanyika ili tuweze kula bila shida na kupunguza kama ukakasi au ule uchungu wake kidogo. Unapopasha au kuzichemsha hizi green beans unaweza kuongeza kiasi kidooogo cha baking powder (tamka; beking'I poouda) ndani ya maji ili kuyafanya maharage haya yasipoteze ile rangi yake nzuri ya ukijani kibichi cha kupendeza.

3. Kata pilipili hoho mara mbili na uondoe zile mbegu mbegu zake za ndani na sehemu zingine zisizohitajika, menya vitunguu na kaloti. Tafadhari, usimenye nyanya wala usitoe mbegu mbegu zake za ndani.

4. Sasa kata kata mboga mboga zako zote katika mkato wa aina moja unaoupenda, kuna mikato ya aina nyingi; unaweza kukata katika duara (rings), pembe nne, pembe tatu, kyubu, na kadharika. Kwa pishi hili mimi napenda zaidi kukata mboga mboga zangu katika julliene (tamka hivyo hivyo; juliene).

5. Kisha kukatakata mboga mgoa zako zote sasa zichanganye pamoja katika bakuli kubwa.

6. Mwisho kabisa iunge salad yako na chumvi, maji/jusi ya ndimu na vijiko 2 u 3 vya mafuta ya zeituni. Tafadhari iunge salad yako (yaani iongeze chumvi, ndimu na mafuta) dakika 1 kabla ya kuandaa mezani hivyo kama umemaliza kuitengeneza na unadhani utahitaji kusubiri robo saa au nusu sasa ndipo ukae ule basi si vema kuiunga papo hapo kwakuwa chumvi itaongeza limchumzi lisilohitajika kwenye salad yetu pia mafuta yataifanya ilainike kiasi inaweza kukera machoni mwa anayekula.

7. Enjoy.

MHIMU:
a. Tumia mafuta ya zeituni (olive oil) tu na si mafuta mengine kwakuwa chakula hiki hakipikwi katika moto na ni mafuta haya tu yanaweza kuliwa bila kupikwa katika moto bila shida yoyote. Kama mahali ulipo huwezi kupata mafuta ya zeituni unaweza kuwasiliana na mimi.
b. Baada ya kukatakata vitunguu, usivioshe au usivisuguwe katika chumvi, kufanya hivyo ni kupunguza thamani ya kitunguu mwilini.
c. Kuna wanaoshikilia kuwa nyanya ziondolewe mbegu mbegu zake katika pishi hili, bali mi nakushauri usiondoe mbegu za nyanya kwani unaondoa lishe mhimu mwilini ndiyo maana utalazimika kuwa na nyanya ambazo hazijaiva sana ili usikereke na hali hiyo.

Utaila na nini hii fresh mixed salad?
Fresh mixed salad ni chakula cha pembeni (side dish) kinachosindikiza chakula kingine kama vile samaki wa kukaangwa (fried fish), nyama choma, au kuku wa kukaangwa (fried chicken) na kufanya mlo kamili ama wa mchana au jioni.

http://fadhili.p.ht/2013/06/fresh-mixed-salad/
 
Back
Top Bottom