Elections 2010 Friends of Dr.Slaa FOD kuhakikisha Slaa anaingia ikulu hatari tupu........

Nimekopi hiyo taarifa kutoka kwenye link hapa chini

"Wana FOS wote,

Kwanza niwaombe radhi kwa kuchukua muda mrefu sana katika kushughulikia suala la kufungua account. Tulichukua muda mrefu kwani kulikuwa na vikwazo kidogo. Ninayo furaha kuwafahamisha kuwa hatimaye tumeweza kupiga hatua muhimu na kufanikisha jambo muhimu sana la kufungua account kwa ajili ya michango ya kufanikisha ushindi wa Mh. Dr. Slaa.

Jina la account ni M4C
Account number ni: 01J108010100600
Benki ni CRDB.

Hivyo, karibuni sana katika kuwakilisha michango yenu kwa kadri ya uwezo wa kila mmoja wetu. Labda kuna mtu atapenda kufahamu kuwa M4C ni maana yake nini? Kwa kifupi maana yake ni Movement four Change.

Pili, napenda kuwafahamisha kuwa nimeongea na Mh. Dr. Slaa amenituma niseme kuwa anashukuru sana kwa moyo wenu na kwa uzalendo wenu mlioonyesha katika kumuunga mkono katika suala hili. Ameguswa sana na juhudi zetu hizi zimempa nguvu sana. Ametiwa moyo sana na hiki tunachojaribu kukifanya.

Kutoka na hilo basi, ametoa mualiko kwa wana FOS wote ili tuweze kukutana sote, tufahamiane, apate fursa ya kutushukuru, tuweze kubadilishana mawazo na muhimu zaidi tuweze kuwaeleza mipango ya FOS na pia kama mna maswali yoyote na michango basi mpate fursa ya kuuliza au kutoa michango yenu ya mawazo.

Hivyo basi, tunapendekeza kukutana siku ya Alhamisi. Muda, mahali na wakati tutafamishana baadae. Kwa sasa Mrs Slaa ambaye anamsaidia Mheshimiwa kuandaa mkutano huu, ameniomba niwasiliane nanyi na ku extend invitation hii kwenu na wale wote mtakaopenda kuhudhuria basi muwasiliane nami katika email yangu mki confirm kuhudhuria kwenu, ili name niweze kumfahamisha ni watu wangapi watakuja.

Nadhani hii ni fursa nzuri sana na ningewaomba tujitahidi kujipanga ili tuhudhurie.

Unaweza kuwasilina nami ku-confirm katika email yangu: srehani@hotmail.com au kwa simu 0756 20 96 66.

Pia nakaribisha mawazo yoyote yale ya kufanikisha mkutano huu muhimu. Kama una wazo usisite kunifahamisha. kuhusu program n.k.

Natanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano wenu katika suala hili. Kwa sasa nahitaji kujua ni watu wangapi watahudhuria???

Asante

Selemani Rehani"

Friends of Slaa
 
Asante The Invincible

Jamani Friends of Slaa FOD wameanzisha Blog yao jaribu kutembelea kuna kila habari unayoitaka kuwahusu wao FOD na zinazomhusu Dr. Slaa mwenyewe. Kama utahitaji gonga hapa

Friends of Slaa
 
Nataka kuchangia mawazo. Mimi ni political strategist, ningeweza kutoa ushauri wa jinsi ya kufanya kampeni nzuri na endelevu. Nina issues nyingi sana zinazofaa kujadiliwa. Suala la wafanyakazi na maslahi yao LISIWE ngao yetu! Kuna mengi zaidi, tena very simple issues lakini ni sensitive na very damaging to the STATUS QUO!
 
SISI WANA FOS TUNADHAMIRIA KUFANYA YAFUATAYO

Kwa hili nawapongeza Chadema wana strategies nzuri na inaonesha kweli wamedhamiria kwenda ikulu keep it up. Kama mipango ndiyo hii lazima CCM wapate wasiwasi.
 
site nzuri sana ina mambo mengi big up waandazi account number tumeiona tutafaza mambo
 

Wangojee Kibano cha wenye hatimiliki Serikali (CCM).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…