Katika mchango wake kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mbunge wa jimbo la Nkenge (CCM) Frolent Kyombo amelalamikia mateso na adha wanayoipata wakazi wa wilaya za Kyerwa, Karagwe, Missenyi na Ngara katika mkoa wa Kagera kufuatia kuwa mpakani na nchi jirani na kuwa baadhi ya watumishi wa idara za Serikali wanatumia kigezo cha lugha na wimbo wa Taifa kubaini nani ni raia na ambaye siyo.
Kuwa wasiomudu vema lugha ya kiswahili au kutoimba vema mashairi ya wimbo wa Taifa wanaelezwa siyo raia wa Tanzania.
Je, wewe unajua vema mashairi ya wimbo wa Taifa au kwa kigezo hicho nawe siyo raia?
Kuna watu siyo raia kwa asili, lakini jambo la kwanza wanajifunza wimbo wa taifa kwa ufasaha. Nimelishuhudia hilo kwa raia kutoka mataifa mawili ambayo ni jirani zetu.
Lakini pia, kuna wazaliwa asilia wa mikoa ya Kagera hasa Karagwe & Ngara hawajui kuimba wimbo wa taifa lkn ni raia.
Waliokosa fursa za kusoma shule walau elimu ya msingi changamoto hii ni kubwa sana.
Kuna waru siyo raia kwa asili, lakini jambo la kwanza wanajifunza wimbo wa taifa kwa ufasaha. Nimelishuhudia hilo kwa raia kutoka mataifa mawili ambayo ni jirani zetu...
Kikitumika kigezo cha wimbo wa Taifa kuamua nani ni raia na ambaye siyo nafikiri itakuwa shida kubwa kwa nchi. Labda kama watu hawajui maeneo mengi ya mashambani hata majina ya viongozi wa kitaifa hawawajui kabisa sembuse wimbo
Wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu, CCM mwaka 2015 pale Jangwani, wasanii waliambiwa kuanzisha wimbo wa Taifa. Waliikimbia Mic hadi alipoichukua Ruby aliyeanzisha kwa mbine bila uhakika. Watanzania wengi hawafaham wimbo wa Taifa.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu, CCM mwaka 2015 pale Jangwani, wasanii waliambiwa kuanzisha wimbo wa Taifa. Waliikimbia Mic hadi alipoichukua Ruby aliyeanzisha kwa mbine bila uhakika. Watanzania wengi hawafaham wimbo wa Taifa.