FROM HERO TO ZERO: Manchester UTD ilifunga goli moja tu katika ligi mwezi uliopita...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Kama bado unaamini kuwa Manchester United bado ni timu kubwa Barani Ulaya basi umepotoka.

Man UTD si klabu kubwa tena na wala sio Man UTD ya kipindi kile iliokuwa inavitisha vilabu pinzani kabla na baada mechi.

Kwa kukuthibitishia hilo, Man UTD kwa mwezi uliopita yaani mwezi Oktoba imefunga goli moja tu katika michezo yake ya Ligi kuu ya Uingereza.

Taarifa hii ni mbaya na haipaswi kumwambia ama kumfikishia shabiki yeyote yule wa klabu hii maana ni habari mbaya na yakusikitisha.


From Hero to Zero…Man UTD ilifunga goli moja tu katika Ligi ya Uingereza mwezi Oktoba…
 
Dah, pamoja na gharama zote hizo za kumleta The Special One, Pogba, Zlatan ? Angalia kumbukumbu zako vizuri bhana ! Hata Titanic haikuzama hivo..
 
Unapomtegemea "mzee" wa miaka 33 kama main striker wako lije jua au mvua, tegemea wanachokipata Man Utd. Mourinho kibri itamponza. Weka bench Zlatan, Pogba na chezesha proven talents ulizozikuta. Kwa rate hii, Moyes anaonekana alikuwa genius na labda mtaalamu Giggs angefanya wonders
 
ila kwenye playstation Ibra anafunga kama yupo dubai mwezi mtukufu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…