''From rags to great riches and honour'' Elevation of the Nation

''From rags to great riches and honour'' Elevation of the Nation

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Likizo yangu ya mwaka huu ilikuwa miongoni mwa likizo bora kama nilivyo tabiri kabla ya hapo.

Kazi zangu ninazozifanya na kunipatia riziki zinanifanya nisitumie muda wangu vyema katika kufikiri hivyo niliamua kuchukua likizo ili mawazo yangu yazame vyema ndani yangu.

Majukumu yangu ilikuwa ni kutengeneza akili yangu katika mambo yafuatayo ambayo kwa hakika ilibidi iwe lazima nitumie moyo wangu wote kuyakamilisha ingawaje mpaka sasa sijayakamilisha ipasavyo kuna baadhi ya mambo yananirudisha nyuma na kuzuia uwezo wa akili yangu ku focus na nguvu zangu kukusanyika ili kupata nguvu ya kukamilisha baadhi ya mambo ambayo na uhakika kama akili yangu ikipata uwezo wa juu wa focus na will power yangu iki increase ipasavyo nitakuwa na uwezo wa kuleta Mapinduzi.

Mapinduzi gani yanayo hitajika katika taifa hili? Ni mapinduzi ya fikra na kujitambua kwetu kama Taifa.

Mabadiliko haya ambayo wote tuna yahitaji ambayo yataleta tija na matumaini kwa wote.


Mtu kabla ya kufanya mission yeyote ni lazima ajijenge kwanza akili yake and spiritual strength ili kukabiliana na changamoto yeyote itakayokuwepo mbele yake. Akiisha fanya uamuzi huu ni lazima awe tayari kufa ili kukamilisha malengo yake na ya jamii yake.

Maono ya kuwa na jamii yenye umoja na endelevu na ya watu wanaoshirikiana ili kuleta maendeleo ya jamii zao na taifa. Haya maono lazima yajengeke akilini mwangu na kwa watu wengine ili tulete mbadiliko.

Jesus christ alienda mlimani na kufunga na kuomba kabla ya kuanza mission yake ya kubadilisha watu kutoka katika uovu, alikusanya watu wengi sababu alijiamini mwenyewe na mungu, alikuwa na hamu ya kuona mabadiliko ya nafsi za watu na alikufa katika heshima mpaka leo watu wana muabudu.

Hakuna mabadiliko yeyote makubwa yatakayotokea katika Taifa hili bila kujitolea Nafsi zetu ili kuona mabadiliko hayo kwa faida ya wote. Kwahiyo tuna hili jukumu mbele yetu la mabadiliko ya fikra kwa watu wetu wote, kujenga watu wetu katika mapenzi kwa Taifa lao na kujenga umoja wa Taifa. Tunatambua bila umoja Taifa letu halitoweza kuwa Imara.

Mabadiliko haya hayawezi kuwa ya kisiasa tu bali pia ya Ki fikra watu wetu katika kila professional lazima wafikirie kuhusu hili kuleta mapinduzi kwa ajili ya Taifa hili wakati wa ubinafsi na kuangalia tumbo tu must end.

Hatutaweza kulisongesha Taifa hili kwa hiyo akili. Ni lazima tuangalie upya mfumo wetu wa elimu na tuwekeze humo. Elimu yetu isiwe elimu ajira tu bali elimu ambayo ita revolutionalize Taifa letu.

Huu ni wito wa kizalendo naamini tunaweza kubadilisha Taifa hili kama kila mtu akiwa muaminifu na mwenye kujitolea. Taifa hili lina muihitaji kila mmoja wetu na kila mmoja wetu anaweza kuleta mabadiliko sehemu aliyopo.

Kama tutakuwa na energy hii na focus na kama tukiamua tunahitaji mabadiliko hakuna kitakacho tuzuia kupata mabadiliko hayo.

Dhana ya kujitegemea lazima iendelee kuwepo ni lazima tujenge uchumi ambao sisi wenyewe tuna umiliki na kutumia vitu ambavyo sisi wenyewe tume vitengeneza kwa mikono yetu. Mambo yote haya yanawezekana kama tuki ji mobilize na kuamua kuleta mabadiliko hayo.

Wananchi ndio wanaoondoa na kuweka serikali nyingine ambayo ita wa suit better itakayoleta tija, matumaini na furaha kwa wote. Pale serikali inapochuja na kuwa ya kifisadi na isiyozingatia utawala wa sheria na common good ya jamii wananchi wana haki ya kuiondoa serikali hiyo na kuiweka serikali nyingine itakayoleta Tija na matumaini kwa wote.

Hii nguvu hii iko mikononi wa kila raia huru wa Taifa hili. Nchi hii inahitaji Dira watu wetu wanahitaji motivation ya kujenga TAIFA lao wenyewe na kujihisi ni sehemu ya taifa.

Hii hisia hii ambayo imekufa miongoni mwa watanzania wengi waliokosa matumaini na wengine kutamani kuzaliwa mbwa ulaya ni roho ambayo itajenga Taifa hili. Kama kila mtu akijua ana hisa katika Taifa hili na haki na anafaidika na uwepo wa serikali yake atatumia nguvu zaidi kujenga Taifa lake kwasababu atakuwa raia anaye thaminiwa. Kila mtu anawajibu kwa Taifa hili na haki zake. Lazima tufahamu hili kwasababu pasipo kufamu hili, Taifa letu halitoweza kusonga mbele. Na Tunahitaji kusonga mbele.

Wakati lazima uje ambao raia na viongozi wanakuwa wamoja wakijenga Taifa lao with courage, hope and perseverance. ''We must have blue print of the Nation we want to build and participate in creation of that Nation'' Nitaendelea kuamini hili Taifa lina uwezo wa kuwa kubwa kama Taifa lolote lile duniani kama tutakuwa na will na kama tuatakuwa wamoja.

kila Taifa lina wa tayarisha vijana wake for the future leadership. hii ndio siri ya kujengeka kwa Taifa lolote kubwa ni jinsi gani tuna watayarisha vijana wetu kwenye uongozi?. Je tuna watengeneza katika Tabia gani? je Tabia hizo zina faida katika future ya Taifa letu? Ni elimu ya aina gani tunawapa? Our LEADERS MUST BE '' BOLD'', men of great courage and prudent. ''Tumaini la taifa lolote linalala katika viongozi wake'' future yake iko katika viongozi wake watu wenye akili wanatambua hili.

Uongozi sio kitu cha mchezo mchezo kama watu wanavyofikiri. Watu wanahitaji haki zao na ulinzi wa ndani na wa maadui wa nje, ni lazima kuwe na rais atakaye hakikisha yote hayo katika effectiveness ya hali ya juu na wakati huo huo kuhakikisha ukuaji wa nchi na Order and stability of the state. Hii inahitaji kiongozi mwenye akili atakaye deal na watu wake vyema. To maintan order in a country it is not an easy thing it need ''mental strength'' Kukimbilia kwenye uongozi kama una mental strength ya kutosha ni kujitafutia matatizo, kutawala watu ni kazi nzito hilo ni jukumu the ''mighty'' You will never keep people in order if you don't have Mental strength to rule and to make people subjected to you and to maintain justice.

Katika Taifa lolote kuna mchanganyiko wa watu wapo wazuri na waovu hujui nani utakabiliana nae na kwa wakati gani kutokana na maamuzi utakayoyafanya ukiwa madarakani. Wengine wanaweza kuwa watu wa karibu yako kabisa katika uongozi ambao wanaweza kubadilisha mwelekeo wako na dira yako ya uongozi. Kuna watu waovu katika dunia hii ambao hawaangalii chochote zaidi ya kujiangalia wenyewe na Taifa linahitaji ulinzi na harmony katika jamii, wananchi wameweka matumaini yao kwako ili uwalinde na uhakikishe haki inatendeka kwa watu wote na Taifa linaendelea.

hii will power, a driving force ambayo ina msukuma binadamu kuleta mabadiliko katika jamii yake sio jambo dogo. Watu wa namna hii lazima waache mambo yao yote ili akili yao na roho yao iwe focus malengo wanayotaka kufanikisha.

Katika Taifa letu tunahitaji watu wa aina nyingi sana watakaoleta mapinduzi lakini bila kujitolea huku kamwe hatutaweza kuleta mabadiliko katika Taifa hili. Huu ni ukweli tunahitaji watu watakaojilea katika nyanja zote. Hii spirit ya pioneer lazima ijengeke. Kama tuna wapenda watoto wetu lazima tuwajengee future yao kama Taifa. Wote tunapenda kuona watoto wetu wakikua katika Taifa la watu wenye umoja na future ya watoto wetu ikiwa secure , kuwa na taifa lenye amani na maendeleo endelevu ili watu wetu waishi bila kuwa na wasiwasi wa kesho atakula nini au atavaa nini. Lakini hii yote inahitaji umoja na collective will ya watu wetu kujiletea maendeleo yao wenyewe bila kusahau uongozi wenye maono na mapenzi mema kwa Taifa.

Kwahiyo future ya Taifa hili itategemea sana elimu tunayotoa kwa watu wetu na kwa vijana wetu. Ni lazima iwe elimu ambayo ita revolutionalize Taifa letu na isiwe elimu iliyojengwa katika misingi ya ajira, Elimu tumbo. Bali elimu itakayomwezesha mwanafunzi kupata maarifa ya kutosha kujitegemea na elimu iliyojengwa katika uzalendo itakayoleta raia wema na wawajibikaji, hili ni tumaini ambalo limelala ndani yangu.

I hope one day our people will be intellegent na kulipenda taifa lao na kuwa tayari kulitumikia na kuliendeleza. I know we can produce great men on the earth right here in our country.

Kwahiyo ni lazima tufikiri kuhusu Taifa hili sasa na mwelekeo wake, kwakuwa hili lina tutegemea sisi. Tuna uwezo wa kukaa chini na kujadili future ya Taifa hili rational, future ya watoto wetu na kizazi kijacho.

Tunahitaji kubadili fikra zetu na ku focus kujenga Taifa hili badala ya kila mtu kujiangalia binafsi. Tumaini langu ni kwamba tutajitambua ya kuwa tuna uwezo na nguvu ya kulinyanyua Taifa hili kutoka hapa lilipo ikiwa tu tutakuwa wamoja na dhamira ya dhati kwa Taifa letu.

Kama tunataka kujenga Taifa hili ni lazima tuwe na blue print ya aina ya Taifa tunalotaka kulijenga hatuwezi kujikulia ovyo ovyo kama mbegu zilizotupwa shambani bila mpangilio lazima kuwe na order na direction. Lazima kuwe na nidhamu bila nidhamu na maadili hatuwezi kujenga Taifa hili. Nidhamu mashuleni, makazini na nidhamu kwa viongozi. We must elevate this nation.

Dhamira yetu ya kujenga Taifa linalojitegemea lazima iendelee with the great courage and perseverence. Lazima tutumie tulivyo vitengeneza kwa mikono yetu wenyewe. We have that power to be great nation. Only we need is the dedication to the Nation. The spirit of pioneer. We must change our mind.

Mwelekeo wa akili zetu wa sasa hauja tufaidisha chochote, mwelekeo wa ubinafsi na kuangalia kila kitu katika umimi. Ni lazima sasa tuangaliane na tujaliane na tujenge Taifa letu kwa pamoja.

Ni lazima tujenge vyama vyetu vya siasa katika misingi imara ya demokrasia na katika uzalendo, katika nidhamu na maadili ili kila mwenye uwezo wa kuwa kiongozi aweze kushiriki katika uongozi wa nchi yake bila uwoga wa kuvunjiwa heshima yake kwa matusi au uoga juu ya maisha yake. Hivi vyama lazima vishindane kwa mawazo na katika uzalendo na kwa hoja na sio propaganda kwakuwa sisi ni wamoja na hatma yetu ni moja.

Ni lazima tuendelee kujenga umoja wetu wa makabila, mikoa na dini. We must build our country in a very strong unity. Na ni lazima twende pamoja with courage and perseverence kujenga taifa tunalohitaji. I do demand unity and leadership in this nation in order for us to move foward.

Imani kati ya viongozi na wananchi lazima ijengwe upya hatuwezi kujenga Taifa hili pasipo imani hiyo. Mwelekeo tunaoenda nao kama Taifa sio sahihi na wala sio bora. ''We need a change of mind and heart''. I see future so bright for us if we wake up kutoka usingizini na kutambua kikwazo chetu ni kutokuwa wamoja kwetu, kutokuwa na nia moja na dhamira moja. ooh watu wa Taifa hili mna baraka ya mungu kwa kila resources kwenye kila ncha ya taifa letu, we can change that wealth to material prosperity only if we are one people and with the one aim na kama tutatumia nguvu zetu na akili zetu kuleta mabadiliko.

We must be one and we must attempt with the courage and perseverance we can change this Nation from rags to great riches. Siwezi kudanganya hii inahitaji kujitolea kizazi baada ya kizazi.

Tunaomba mungu rehema zake na ulinzi wake kwa Taifa hili ili ardhi yetu iendelee kuzalisha na watu wetu wajitambue wao ni kina nani ili taifa letu lipate mwekekeo na heshima. Hatuwezi kuendelea kuwa Taifa ombaomba na maliasili kibao ziko pembeni yetu. Nawaomba mfikiri sana ukombozi wa taifa hili uko mikononi mwenu. Bila kufikiri Taifa hili halitoweza kuendelea.

Katika maisha yote busara amekuwa mlinzi na muendelezaji wa mataifa lakini ujinga umeharibu na kuangamiza mataifa. Tuna uwezo wa kupata busara hii ili tujenge na kulilinda taifa hili na mwelekeo wake uwe endelevu na wenye tija kwa watu wote.

Nawatakia mafanikio mema katika maisha kila mmoja wenu na katika kulipenda taifa lenu na muwe na akili zinazoona na kufikiri nje ya ubinafsi ili Taifa letu liende mbali. Changamoto zetu ni zetu na ni jukumu letu kuziondosha. Kila mmoja wetu anaweza kujenga heshima ya Taifa hili.

Tunaomba uangalizi wa mungu macho yake yawe kila siku juu ya Taifa hili na watu wake atu bariki na kutulinda kwa kila lililo jema.'' I hope and i believe'' in whom who create everything, in God i trust.
 
Na hiki ndio kipimo cha Mabadiliko ya Fikra "NI kwa makanisa na misikiti kufugiwa nguruwe, kuku, ng'ombe, ama kuwa madarasa ya ufundi na juzi mbalimbali" Ni laziwa "TUJIKATAE" kuonesha kwamba tuko hai kifikra, maana kila kitujengacho leo kimeoza kinanuka, ni UPUUZI kwani kimezaliwa na kukuzwa na HULKA zetu, si MANTIKI iliyomo ndani yetu!
MAISHA NI FURAHA, KAMA HAIPO MAISHA NI UPUMBAVU MKUBWA. NA HAKUNA FURAHA YA MTU ILA WATU. Na hiyo ndio MANTIKI, yaani UTU!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Na hiki ndio kipimo cha Mabadiliko ya Fikra "NI kwa makanisa na misikiti kufugiwa nguruwe, kuku, ng'ombe, ama kuwa madarasa ya ufundi na juzi mbalimbali" Ni laziwa "TUJIKATAE" kuonesha kwamba tuko hai kifikra, maana kila kitujengacho leo kimeoza kinanuka, ni UPUUZI kwani kimezaliwa na kukuzwa na HULKA zetu, si MANTIKI iliyomo ndani yetu!
MAISHA NI FURAHA, KAMA HAIPO MAISHA NI UPUMBAVU MKUBWA. NA HAKUNA FURAHA YA MTU ILA WATU. Na hiyo ndio MANTIKI, yaani UTU!

Kwanini makanisa na misikiti ifugiwe nguruwe? Mimi nafikiri watu wetu wanahitaji dini kama makanisa na misikiti imekosa mwelekeo inabidi tutafakari kuhusu hilo pia ni jinsi gani tutayarudisha katika mstari. Dini zinajenga maadili ya watu ni muhimu sana kwa Taifa. Tunahitaji waumini wazuri wa dini ili kujenga Taifa la watu waadilifu na wanyenyekevu.

Kuhus furaha ni sahihi katika Taifa kujenga furaha ya pamoja. Taifa ambalo kila mmoja ana thaminiwa utu wake.

Nadharia yako kuhusu hulka na mantiki nimeipenda sana na umenipa majina ya kutumia. Ninachojua hulka hutumia zaidi wanyama ambao hawana fikra kuna huiki kitu kinaitwa impulses ambacho ni lazima kiwe regulate ili reasom isihike hatamu yake badala ya hiyo hulka. Nafikiri ndio hasa lengo la elimu ya kwamba binadamu atumie fikra na mantinki zaidi ya hukra ambayo kawaida haijengi.

Madarasa ya ufundi na ujuzi mbali mbali ni muhimu kujengwa sio kujengwa tu lakini watu wajengewa spirit ya uzalishaji na uzalendo wakijua kwamba wanashiriki katika ujenzi wa Taifa lao. Ni lazima tuondoe huu ubinafsi kama tunataka kuendelea. ili akili zetu zielekezwe kwenye ujenzi wa Taifa hili. Tutakuwa na furaha kama tutafanya kazi kwaajili ya Taifa ili kupata mafanikio ya pamoja ingawaje kila mmoja wetu ana haki na uhuru wa kuwa na mali zake lakini pia anawajibu kwa Taifa na jamii katika vitu hivi viwili lazima kuwe na harmony kati ya wajibu binafsi na uke wa Taifa.

Inabidi tuangalie upya pia kuhusu watumishi wa umma na uwajibikaji wao kwa jamii na tujenge upya uzalendo kwao na roho ya kutumikia. Ikiwa kila mtu akitia juhudi kwa kila alitendalo kwa manufaa binafsi na yale ya Taifa tutafika sehemu.

Naheshimu sana kuhusu dini na nisingependa dini iondoke miongoni mwa wanadamu kwakuwa dini hubadilisha mienendo yetu. Iam firmly believer in God of the Bible and his promise of redemption to all man kind, i rest my hope in him and my strength.

Fikra zako kuhusu hulka nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa sana na huo ndio ukweli.

Nakutakia kila la kheri .
 
Back
Top Bottom