Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Kila mtu ana historia ya maisha yake. Hakika kupambana ndiyo njia pekee ya mafanikio, lakini kupambana kwa mwanamke inaweza ikawa ni kama kuteleza tu juu ya ganda la ndizi, hasa kutokana na uzuri wa umbo au sura. Uzuri imekuwa ni kama passport na visa ya kufikia mafanikio kwa wadada walio wengi.
Vyovyote iwavyo kila mwanadamu ana historia, kila mwanadamu ana mahali pa kuanzia na akifika pale alipopatamani siku zote kule alikotoka huwa inabakia kuwa ni historia tu. Haijalishi ni namna gani umefika, iwe ni kwa kubebwa, kwa kujibeba, kwa kupambana, au bahati tu, yote ni mafanikio.