From scratch: Jinsi ya kuwa dalali popote pale ulipo.

From scratch: Jinsi ya kuwa dalali popote pale ulipo.

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Eeeh wakuu,

Leo nitavunja code ya udalali kwa watu wote ambao wanalala hawajui wakiamka waende wapi wakatafute ridhiki. Hii code kanipa jamaa aliyekuja huku bariadi kwa ishu zake namimi nimeona niwape bure.

NILIMUULIZA ULIANZAJE ANZAJE KAZI YA UDALALI

Akanijibu short tu, "nilishikwa mkono na rafiki yangu akanifundisha udalali,

Hili jibu sikulielewa nikamuuliza ulianzaje anzaje kuwapata wateja je mlikuwa mnaenda na rafiki yako pale mteja anapopatikana? Akajibu hapana. Kiukweli nikawa sinuelewi ikabidi nimbadilishie swali


KWA MFANO UMEHAMIA MKOA MPYA MKOA X NA KTK HUO MKOA WEWE NI MGENI JE UTAANZAJE ANZAJE KAZI YA UDALALI?

Akanijibu kitu cha kwanza atatengeneza mabango (yale ya kubandika kwenye nguzo miti au ukuta yale ya karatasi) bango litajieleza dalali wa nyumba, viwanja n.k bango litakuwa na namba za simu.

Kitu cha pili atatengeneza vipeperushi atavigawa sehemu mbali mbali vijiweni na kwenye mikusanyiko ya watu

Kiukweli hili jibu nikaona lina sound vizuri japokuwa sio geni ni jambo ambalo watu wengi wanalifanya ila ghafla likanijia swali jingine kichwani

KWA MFANO UKAPATA MTEJA WA CHUMBA AU KIWANJA AKAKUPIGIA SIMU JE CHUMBA AU KIWANJA UTAKITOA WAPI ? MAANA WEWE UTAKUA MGENI!

Akanijibu baada ya kubandika mababgo na kusambaza vipeperushi atawatafuta madalali wote wa lile eneo alipo yeye atachukua namba zao kisha atashirikiana nao (kula nao)

Hivyo basi yeye akipigiwa simu na mteja amnamsikiliza kisa na yeye anavuta waya kwa wale madalali wenyeji anapatanisha kisha ndio anampereka huyo mteja

Ikabidi nicheke kwanza 😀 hapa niliona ni ujanja ujanja huu mjini akili ni mtaji kijijini mtqji ni nguvu.

NB: watu kukupigia simu (wateja) ni suala la kiroho pia wale wa kanisani kabla hujaanza unatoa sadaka church, wale wa msikitini ynamfuata shehe anakusomea dua na unatoa sadaka, wale wa kwa babu unaenda kijijini kwenu kuaga, wale wapagani unaanza hivyo hivyo kibishi kikubwa kila mtu na imani yake.


Nakaribisha shuhuda na story mbali mbali namna ulivyoanza udalali au mtu unayemjua jinsi alivyo anza ili watu humu wajifunze na wajikwamue kiuchumi

Nawasilisha
 
Kweli maisha ni magumu
Mimi mkuu nimefanya kushare leo nimepata ka muda baada ya kutoka kutizama mechi yetu pendwa ya yabga na Mazembe

Mawazo kama haya usiyadharau mkuu jamaa yupo kwenye udalali kwa miaka kumi sasa ana mke na watoto na amejenga nikaona sio dhambi kujua kitu kipya
 
Mpaka mkubwa wa nchi na mawaziri wake,wanadalalia deal kibao
Mtu hawezi shindwa kwenda ulaya kumleta contractor au muwekezaji aje ila yeye atapewa 10 percent na huyo contractor akija atapewa kazi

Huo udalali ni wa wakubwa mkuu unaitwa kibobgo bobgo UFISADI
 
Back
Top Bottom