Frusa za biashara kwa vijana wa kitanzania

lyalya

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
602
Reaction score
555
Ndugu wana jukwaa poleni na shughuli na majukumu ya kila siku.
Nianze moja kwa moja kuhusu mada iliyo tajwa,Kwa vijana wa kitanzanzia ambao wanajituma kila
siku ili kuhakikisha maisha yanaenda mbele mwaka 2012 Waziri wa kipindi hicho Mh.Samuel Sitta
aliwasihi vijana wa kitanzania waache kulalamika bali wachangamukie fursa za biashara zilizo kuwepo kwenye Taifa changa la Sudani Kusini sasa huu ni mwaka wa saba tangu tutangaziwe fursa hizo ila kwa utafiti nilioufanya kuna vijana wengi kutoka mataifa jirani zetu (Uganda & Kenya)
wamefanikiwa kutokana na fursa hizo lakini sijapata mrejesho kutoka kwa Watanzania wenzangu mambo yao yanaenda je huko,
Ndugu zangu naomba mwenye kujua lolote kuhusu biashara ndani ya Taifa hili changa Barani Afrika atupe taarifa.
 
nimefahamishwa kwamba kuna vijana wa kitanzania wasiopungua 50 wanafanya shughuli mbalimbali za biashara nchini sudan kusini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…