FT: AFCON Qualification 2025: Kenya 0-0 Zimbabwe | 06.09.2024

FT: AFCON Qualification 2025: Kenya 0-0 Zimbabwe | 06.09.2024

Tembosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,487
Reaction score
3,978
Screenshot_20240906-161408~2.png

Duke Abuya Vs Prince Dube.

Game On...
33'
Mpira unaendelea kwa kasi sana.
Duke Abuya kiungo anaubonda sana leo

35'
Kenya wanajitahidi kufika kwenye lango la Zimbabwe wanakaa imara pale.

36'
Dube anatoa pasi nzuri inaleta shambulio kali kwenye lango la Kenya.
Inaokolewa, Kenya wamekoswa koswa hapa.
Namna gani pale.

39'
Zimbabwe wanaingia tena kwenye box la Kenya, shambulizi linakuwa ndogo.
Biliant Anapewa Kadi ya Njano.
Kenya wanajitahidi kuzuia mashambulizi ya Dube.

41'
Dube anapiga shuti kali linaishia kwenye mikono ya Kipa Onyango wa Kenya.
Kenya wanaruhusu mashambulizi ni kama vile kiungo yao inakatika.

43'
Kenya wamefika kwenye lango la Zimbabwe shambulizi limekuwa dhaifu.

45'
Zimeongezwa dakika 3.
Kukamilisha kipindi cha kwanza.

HT
0-0
Screenshot_20240906-165626~2.png


=========================
UPDATES 2ND HALF

46'
Kenya wanapata kona, inapigwa haileti madhara kwa Zimbabwe.
Game On 0-0

50'
Yellow Kadi inatoka kwa Odada wa Kenya, kucheza rafu kwa mchezaji wa Zimbabwe.

52'
Kenya wanafika langoni kwa Zimbabwe, ila wanafanya uchoyo mambo hayaendi hapa.
Wanaforce penalty refa anakataa.

54'
Kenya wanapata kona nyingine lakini haizai matunda!!

56'
Kenya wanapata kona nyingine, anaanza kona fupi lakini inaokolewa na Wazimbabwe!
Hadi sasa 0-0

57'
Kenya wanafanya mashambulizi kwa Zimbabwe, mpira unatolewa inakuwa kona
Zimbabwe wanafanya Sub kabla kona kupigwa.
Kona inapigwa linatokea shambulizi halijaleta impact.
Kipa wa Zimbabwe anapata jeraha anapatiwa matibabu.
Inaonekana anaweza kuendelea.

60'
Game On...
0-0

61'
Dube anakosa goli hapa. badala yakufunga yeye anatoa assist.

64'
Mpira umesimama kidogo baada ya wachezaji wawili kugongana.
Wamechezeana faulo.
Watoa huduma ya kwanza wanawapa msaada.

Takwara wa Zimbabwe anapata yellow Kadi.

67'
Game on...
Harambee stars wanafika kwenye box.
Umaliziaji unakuwa butu.
Wakati huo Kenya wanafanya mabadiliko ya wachezaji wao.

68'
Kenya wanapata tena kona hapa.
Inapigwa haileti shida kwa Zimbabwe

71'
Zimbabwe wanapata kona.
Inapigwa hapa vizuri, goli kipa Omondi anadaka.
Game On...
Kenya wanamiliki mali sasa.

77'
Bado hakuna mashambulizi yakutisha kwa timu zote mbili.

78'
Zimbabwe wanapata kona nyingine hapa inapigwa.
Inakuwa dhaifu, Kenya wanaosha.

81'
Zimbabwe wanafanya sub yao ya nne hapa.
Game on
0-0

83'
Kenya wanafanya shambulizi kali langoni mwa Zimbabwe lakini Inaishia kwenye mikono ya Goal Kipa wa Zimbabwe.
Game on...Kenya wanatembea hapa.

86'
Kenya wanafanya mabadiliko ya wachezaji wake wawili hapa.
Game on Kenya side now.

90'
Game On.
Bado milango migumu.
Dakika 4 zimeongezwa.

90+3'
Zimbabwe wanafanya shambulizi kali langoni mwa Kenya.
Ila hawapati kitu zaidi ya kona.
Inapigwa kona inaokolewa hapa.

FT
Kenya 0 - 0 Zimbabwe
 
Nitatoa updates kwenye post #1
 
Hawa wachezaji wazimbabwe namna walivyo maveteran ilitakiwa Kenya iwe inaongoza hata goli 3 kipindi Cha kwanza
 
Huu Uwanja wa Nelson Mandela Nambole Uganda ni mzuri sana
 
Prince Dube.
Anatoa assist kwenye 6' 🤣
 
Back
Top Bottom