FT: Al Akhdar 3-0 Azam FC / Confederation Cup / October 8, 2022

FT: Al Akhdar 3-0 Azam FC / Confederation Cup / October 8, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Full time

Anakosaaaaaa, kipa wa Azam FC anapangua penati.
90' Al Akhdar wanapata penati.
87' Shambulizi la Al Akhdar mpira unagonga nguzo.

63' Wenyeji wanamiliki mpira na kufanya mashambulizi kadhaa.
50' Azam wameonesha utulivu, mchezo umepungua kasi.

Kipindi cha pili kimeanza

Mapumziko, Azam FC wapo nyuma kwa magoli matatu.

45' Wapinzani wa Azam FC wanacheza soka la kasi na kuwafanya wageni wafanye makosa mara kwa mara.

25' Kasi ya mchezo iko sawia, timu zinashambuliana kwa zamu.
16' Mchezo unasimama kwa muda, mashabiki wa Al Akhdar wanarusha chupa kwa mwamuzi wa pembeni.
15' Al Akhdar wanaweka mpira wavuni lakini inakuwa offside.
11' Gooooooooo, wanafunga goli kwa mkwaju wa penati.
10' Penatiiiiiiii, wenyeji wanapata tuta iliyotoka na faulo.
5' Azam FC wanacheza kwa utulivu.
Mchezo umeshaanza.

Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC ipo ugenini kucheza dhidi ya Al Akhdar ya Libya.
View attachment 2380939
 
Hawa goli la tatu linakuja...ni muda tuu. Ngoma inamalizika huko huko ugenini. Return leg ni kukamilisha ratiba
 
Ndugu zao Simba wamezoea kukalia tano tano wakiwa ugenini.
Simba ni lidude kuubwa linapokuja suala la kimataifa.

Utopolo a.k.a mavi fc mtaumia sana.
Kwenye ranking Simba ni ya 12 wakati utopolo ndani ya 75 bora Afrika haimo.

Endeleeni kununua tu mechi za hapa mkisaidiwa na baadhi ya wapiga dili kwenye vilabu vyetu vya ndani
 
Kipind cha pili azam wabadili mbinu zao la sivyo anakufa 5
 
Hawa jamaa mpira wao ni kasi ila hawana maajabu .azam akipata goli moja tu akija chamazi anakufa nyingi. Kocha wa azam ni muongo kwann asiende na mshambuliaji mmoja ili kuheshimu timu pinzani.
 
Hawa jamaa mpira wao ni kasi ila hawana maajabu .azam akipata goli moja tu akija chamazi anakufa nyingi. Kocha wa azam ni muongo kwann asiende na mshambuliaji mmoja ili kuheshimu timu pinzani.

Mkuu hilo ndio wanasema mashabiki wa yanga kwamba wakienda kule Sudan wataenda kushambulia tu,kitawakuta kama azam,ukiwa ugenini wewe kaa nyuma unashambulia kwa machale.

Wanafikiria wanacheza na ihefu hapo, hapo ni kimataifa,sio tu kupeleka mpira mbele.
 
Tatizo Yanhga wanacheza kwa kulinda legacy

Wanacheza ili wasifungwe, hawachezi ili washinde

Kwao mahesabu ya mechi sio katika point tu, bali hadi ile rekodi ya kutofungwa bado wanataka kuendelea kuienzi.

Nadhani kwenye mechi ya marudiano Nabi lazima acheze Jihad na hapo ndipo utaona timu ikicheza vizuri hata kama itatokea wametolewa ila kivyovyote vile wataluwa wamecheza vizuri kuliko walivyo cheza leo
 
Mkuu hata leo kipa wa yanga ndio man of the match,sasa hiyo inaosha yanga walikuwa wanakoswakoswa na kipa anaokoa,

Ukicheza vizuri halafu ukafungwa inakuwa vizuri kujia mapungufu yako.

Yanga wajaonesha ile hali ya kuwa tuko nyumbani.
Walikuwa wako slo sana,nadhani anakosa uzoefu.

Kila kitu walitakiwa wa alakishe.sijajua yanga watakuja na uchezaji wa namna gani ili wapate matokeo,
Africa kila timu inashinda nyumbani kwake,sasa usiposhinda nyumbani hivi kule uwezekano ni mdogo.
 
Back
Top Bottom