FT: Azam FC 0-2 Simba SC | NBC Premier League | Azam Complex

Hongera sana mtani kwa kuokota alama tatu muhimu sana msimu huu. Hakika nyota njema huonekana asubuhi. Mna kocha mzuri sana awamu hii
 
Yanga huwa wanashinda kwa kutukabia juu na kwa sababu huwa tunafanya makosa wanatufunga, ikitokea tu kocha akategua huo mtego tutawafunga.
Na hatuwaachii, tutawakabia hukohuko juu!
 
Reactions: Tsh
Nikisema Simba wana team, wananchi wenzangu wananipopoa, bahati mbaya nimekosa hii game niko safarini ila najua tu mnyama mwenye hasira ameendelea kurarua viumbe huko.

Na tusipobadilika, safari ijayo Simba wanalipiza machungu yao yote.
HAITATOKEA. NAKUAPIA. CHINI YA MAMA YANGA TUPO VIZURI SANA
 
HAITATOKEA. NAKUAPIA. CHINI YA MAMA YANGA TUPO VIZURI SANA
Mkuu naomba urekebishe hicho kiapo, umeenda mbali sana. Kuna jamaa hua anasema kuna vitu vitatu haviaminiki na vinawezakukuaziri mbele ya watu wakati wowote.

1. Mpira (matokeo yanaweza kukushangaza)
2. Siasa (Mabadiliko yasiyotarajia ni jambo la kawaida)
3. Muhogo (unashangaa wakati unauonja mbichi, ulikua sawa, unaupika, unakua mchungu au hauna unga, mgumu).

Simba wameshajipata kama team licha ya kasoro ndogondogo.
Sie tumewekeza sana lakini bado sijaona mpira wa kutakata unaoendana na nguvu iliyotumika.
 
Yatujenge vipi? Refa anatuumiza wazi wazi? Em kuwa serious?
Huwezi rudi nyuma ukafuta kutokuumizwa, option iliyobaki ni kuimarika zaidi ya ulivyokuwa wakati unaumizwa.
 
Ibenge ni bonge la kocha. Wachszaji ndio walimdissapoint Himid Mao anapiga buti badala ya kucheza boli
Yule refa na wasaidizi wake wote ni wa kufungiwa. Huyu jamaa kacheza rafu hatarishi zaidi ya nne kipindi cha kwanza lakini hakupewa kadi hata moja. Kama refa na wasaidizi wake hawakuziona rafu zote nne basi huenda wana matatizo ya macho au uwezo wao wa kutafsiri sheria utakuwa na walakini. Kadi kaja pewa kipindi cha pili baada ya kucheza rafu nyingine. Siku akija kumvunja mchezaji mwenzie uwanajani ndio utasikia kila mtu anampigia kelele wakati huu upuuzi anafanya kila mechi na watu wapo kimya kama vile hajafanya kosa. Na hapo utakuja kumuona huyo huyo Mao naye anaenda hospitali kutoa pole kwa aliyemvunja kama vile itakuwa ni bahati mbaya wakati ndio michezo yake ya kila siku ya kudhamiria kuwaumiza wenzake.

Ni mtizamo tu
 


HII NCHI NI YETU NIAMINI MIMI. HAKUNA WAKUTUZUIA KUCHUKUA UBINGWA. SIMBA WAPAMBANE WAWEZAVYO ILA HAITATOKEA. YANGA BINGWA
 
Simba ni bingwa wa kihistoria, Afrika na Ulaya wanaijua Simba na Si hizo za kijanini na manjano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…