FT || Azam Fed Cup: Yanga S.C 7-0 Rhino Rangers: Uwanja Benjamin Mkapa

mzee wa bwaksi

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,255
Reaction score
3,972
Ni Jumapili nyingine tena tunakutana katika mpambano wa kukata na shoka ambapo mabingwa watetezi wa Azam Federation Cup, Young Africans wanashuka uwanja[emoji2522] wa Benjamin Mkapa kuwakaribisha Rhino Rangers kutoka Tabora.

Ikumbubwe mechi hii ni ya mtoano kuelekea 16 Bora na mshindi lazima apatikane.

Je ni Yanga [emoji617] au Rhino[emoji1661] Rangers ndio wataibuka washindi baada ya dakika 90?

Muda wowote mpira utaanza hapa katika dimba[emoji2522] la mkapa


"""""""""'''''''''
00' Kipyenga kimepulizwa tayari kushiria kuanza kwa mtanange huu

02' Yanga [emoji617] wameanza kulisakama mapema sana lango la Rhino Rangers mashambulizi makali yanaokolewa na golikipa wa Rhino

07' Gooooal[emoji460] Dickson Ambundo anawatanguliza Wananchi mapema kabisa

16" Gooooal[emoji460][emoji460] Kennedy Musonda anaweka kambani goli la pili kwa Yanga

19' Aziz Kiiiiiiiiii[emoji460][emoji460][emoji460] anaweka goli la 3 Kwa Yanga

23' Gooooal [emoji460][emoji460][emoji460][emoji460] Farid Mussa anafunga goli la 4 Kwa Yanga

27' Goooal[emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ni goli la 5 Kwa Wananchi[emoji617]. Mfungaji ni Yanick Bangala

45+2' Dakika mbili za nyongeza Yanga bado wanalisakama kama nyuki lango la Rhino Rangers
Naam mpira ni mapumziko Wananchi [emoji617] wanakwenda vyumbani wakiwa mbele Kwa magoli ma 5 kwa bila

Kipindi cha pili kimeanza

45' Goooal[emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460] Kennedy Musonda anashindilia msumari wa 6 kwenye jeneza la Rhino Rangers

90' Gooooal [emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji119][emoji119][emoji119]David Bryson anafunga goli la 7 Kwa upande wa Yanga

Dakika 90 zimetamatika hapa Uwanja[emoji2522] wa Benjamini Mkapa ambapo mabingwa [emoji471] watetezi wa Azam Federation Cup Yanga [emoji617] wanaondoka na ushindi mnene wa goli 7-0 na kusonga mbele hatua ya 16 Bora.
Tukutane next time[emoji122][emoji122]


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…